Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-08 16:11:54    
Usimamishaji wa vita kati ya Palestina na Israel vyakabiliwa na changamoto

cri
    Watu wenye silaha wa Palestina tarehe 7 walipiga mizinga dhidi ya makazi ya wayahudi kwenye ukanda wa Gaza, mfanyakazi wa China na mwingine wa Palestina waliuawa kutokana na mashambulizi hayo, na wengine 6 wa Palestina walijeruhiwa. Siku hiyo, watu wenye silaha wa Palestina walipambana vikali na jeshi la Israel, na wapalestina wawili waliuawa katika mapambano hayo. Matukio hayo yaliyofanyika mfululizo yanafanya usimamishaji vita kati ya Palestina na Isarel ukabiliwe na matatizo.

    Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa, siku hiyo, watu wenye silaha wa Palestina walirusha makombora na roketi kwa makazi ya wayahudi yaliyoko kwenye ukanda wa Gaza, kombora moja lilipigwa kwenye banda kubwa la kilimo kwenye makazi hayo, na kuwajeruhi na kuwaua wafanyakazi wa China na Palestina waliokuwa wakifanya kazi huko.

    Balozi mdogo wa China nchini Isarel Bw. Fan Jianmin alieleza kuwa, mfanyakazi wa China aliyeuawa anaitwa Bi Shude, ambaye anatoka Tonghua mkoani Jilin, China alikuwa na umri wa miaka 45. Bw. Fan alisema kuwa, baada ya kupata habari hiyo, ubalozi uliwasiliana na polisi na hospitali ya Israel, ili kuthibitisha hali halisi ya watu hao waliouawa. Habari zinasema kuwa, maiti ya Bi Shude itasafirishwa kwenye kituo cha ukaguzi wa maiti huko Tel Aviv, na ubalozi wa China umewasiliana na kampuni ya bima, ili kujadili suala la fidia kwa watu hao waliouawa. Kampuni ya bima ya umma ya Isarel itatoa fidia kutokana na hali ya familia ya watu hao waliouawa. Baada ya tukio hilo kutokea, mwendeshaji wa banda la kilimo kwenye Ukanda wa Gaza alieleza kuwa, wafanyakazi wengi wa huko ni wapalestina na wathailand, na wachina ni wachache sana, Bi Shude aliuawa kwa bahati mbaya.

    Habari zinasema kuwa, wachina wanane waliuawa kwenye migogoro kati ya Palestina na Israel tokea mwaka 2002. Tarehe 12, Aprili, mwaka 2002, mlipuko wa kujiua ulitokea kwenye kituo cha mji wa Jerusalem, na wafanyakazi wawili kutoka mkoa wa Fujian wa China waliuawa. Tarehe 17, Julai, milipuko miwili ya kujiua ilitokea kwa mfululizo huko Tel Aviv, na wafanyakazi wawili kutoka mkoa wa Fujian waliuawa. Tarehe 5, Januari, mwaka 2003, wafanyakazi wengine watatu waliuawa kwenye mlipuko wa Tel Aviv.

    Radio ya Israel imeripoti kuwa, Kundi la Jihad la Palestina limetangaza kuwajibika na tukio la upigaji wa mizinga yaliyotokea tarehe 7 kwenye Ukanda wa Gaza, na kusema kuwa, kitendo hicho ni kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa jeshi la Isarel kumwua kiongozi muhimu wa kundi hilo. Kundi hilo pia limeeleza kuwa, kitendo chake cha kulipiza kisasi kitaendelea. Habari zinasema kuwa, kitendo hicho cha Jihad kinatokana na kitendo cha kijeshi kilichochukuliwa na jeshi la Isarel dhidi ya kundi hilo. Tarehe 7 asubuhi, askari wa jeshi la Isarel waliingia katika kijiji cha Kabatiya, kilichoko kusini mwa Jenin, na kujaribu kumkamata kiongozi muhimu wa kundi la Jihad la Palestina kwenye sehemu hiyo Bw. Mraweh Kmeil. Katika kitendo cha usakazji, jeshi la Israel lilimwua Bw. Kmeil , na kumwua mpalestina mwenye silaha, na watu wengine 5 walijeruhiwa.

    Kwa kweli, mgogoro kati ya kundi la Jihad na Jeshi la Isarel umedumu kwa muda mrefu. Tangu viongozi wa Palestina na Israel wasaini makubaliano ya kusimamisha vita mwezi Februali, mwaka huu nchini Misri, ingawa kundi la Jihad lilipokea makubaliano hayo kwa maneno, lakini halikukubali kwa moyo wa dhati. Baada ya kufikiwa kwa makubaliano hayo, wanachama wa kundi hilo walizusha mlipuko wa kujiua huko Tel Aviv, na kuwaua watu 4. Baada ya hapo, Isarel ilitilia mkazo mapambano dhidi ya kundi la Jihad.

    Habari zinasema kuwa, Bw. Abbas ataelekea kwenye ukanda wa Gaza, na kuwa na mazungumzo na kiongozi wa kundi la upinzani la kiislamu la Palestina Hamas, ili kuzuia hali ya wasiwasi isizidi kuwa mbaya.

    Habari nyingine zinasema kuwa, mnadhimu mkuu wa jeshi la ulinzi wa Isarel Bw. Dan Halutz tarehe 7 alisema kuwa, hivi sasa jeshi la Isarel halina mpango wa kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya watu wenye silaha kwenye makazi ya wayahudi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-08