Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-08 16:40:08    
Mapishi ya Mapo doufu

cri

Mahitaji

Doufu gramu 400, nyama ya ng'ombe ya kusagwa gramu 200, kiasi kidogo cha vipande vya vitunguu maji, tangawizi, vitunguu saumu, sosi ya pilipili, pilipili manga, chumvi, mchuzi wa soya, maji ya wanga, sukari na mafuta.

Njia

1. kata doufu iwe vipande, vipakue ndani ya bakuli moja, mimina maji ya uvuguvugu halafu vipakue na uvikaushe.

2. tia mafuta ndani ya sufuria pasha moto mpaka yawe nyuzi joto asilimia 60, tia nyama ya ng'ombe ya kusagwa, korogakoroga halafu tia vipande vya tangawizi, vitunguu saumu, sosi ya pilipili na chumvi, korogakoroga mimina maji ya uvuguvugu na tia vipande vya doufu, punguza moto kidogo baada ya kuchemsha, tia sukari, mchuzi wa soya, na M.S.G, mimina maji ya wanga, korogakoroga polepole, ipakue ndani ya sahani na kisha utie pilipili manga. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.