Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-08 20:19:53    
Mkoa wa Henan China kutekeleza utaratibu wa kuripoti matukio ya Ukimwi kwenye mtandao wa Internet

cri

Kuanzia tarehe mosi mwezi Julai mwaka huu, mashirika ya tiba kuanzia ngazi ya wilaya mkoani Henan, China yanatakiwa kuripoti moja kwa moja matukio ya ugonjwa wa Ukimwi kwa njia ya mtandao wa Internet yakigundua watu walioambukizwa au wanaoshukiwa kuambukizwa virusi vya Ukimwi na wagonjwa wa Ukimwi.

Imefahamika kuwa, zamani idara za tiba ambazo ni pamoja na hospitali na mashirika ya upimaji mwili na kinga zilipogundua watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi na wagonjwa wa Ukimwi waliripoti matukio hayo kwa kupiga simu, halafu watu wa shirika la udhibiti wa maradhi walikwenda kukusanya hali halisi ya walioambukizwa na Ukimwi.

Kuanzia tarehe mosi mwezi Julai, mkoa wa Henan utatekeleza utaratibu wa kuripoti kesi hizo moja kwa moja kwenye mtandao wa Internet, mashirika husika yakigundua watu walioshukiwa au kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Ukimwi na wagonjwa hayana budi kujaza kadi maalum na kuripoti moja kwa moja kwenye mtandao wa Internet.