Wawakilishi wa Korea ya kusini na Marekani hivi karibuni walifanya mawasiliano mara mbili kwa kupitia "njia ya New York". Ingawa pande hizo mbili bado hazikupata maendeleo makubwa katika kufikia maoni ya pamoja kuhusu kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea, lakini dalili zote zimeonesha kuwa, kuna matumaini ya kuanzishwa tena kwa mazungumzo hayo.
Kufanya mazungumzo kati ya Ofisa wa Marekani na mwakilishi wa kudumu wa Korea ya kaskazini katika Umoja wa Mataifa ni njia pekee ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Korea ya kaskazini na Marekani kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea. Ingawa serikali ya Bush inashikilia kutopitia mazungumzo ya pande mbili hizo, ili kutatua suala la nyuklia la peninsula ya Korea, lakini wachambuzi wanaona kuwa, pande hizo mbili zilikuwa na mawasiliano mara mbili tarehe 13 Mei na tarehe 6 Juni, hii imeonesha kuna mawasiliano ya kiasi fulani kati ya pande hizo mbili.
Habari zilizodokezwa zinasema kuwa, mawasiliano kati ya pande hizo mbili huko New York mwezi Mei yalifanyika kutokana na ombi la Marekani. Katika mawasiliano hayo, ofisa wa Marekani alieleza wazi kuwa Marekani inaitambua Korea ya kaskazini ni nchi yenye mamlaka, na Marekani haitaki kuishambulia au kuivamia. Vyombo vya habari vya nchi za nje vinasema kuwa, katika mawasiliano hayo, mjumbe maalum wa Marekani anayeshughulikia suala la nyuklia la peninsula ya Korea aliainisha kuwa, kama Korea ya kaskazini itaacha mpango wake wa nyuklia, itakomesha mara moja hali ya usimamishaji vita kati ya pande hizo mbili, pande hizo mbili zitaweza kujadili kuanzisha utaratibu mpya wa amani ya peninsula ya Korea, na kuufanya uhusiano kati ya pande hizo mbili kuwa wa kawaida. Lakini baada ya hapo Korea ya kaskazini haikutoa jibu kuhusu msimamo huo wa Marekani, ikawa watu wa nje ya pande hizo mbili wakazidi kuwa na wasiwasi. Katika hali hiyo, Korea ya kaskazini ilitoa ombi kwa hiari kufanya mawasiliano tena tarehe 6 Juni, hii imeonesha juhudi za Korea ya kaskazini.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema kuwa Korea ya kaskazini imesema kuwa inapenda kurudi tena katika mazungumzo ya pande 6, lakini haikuthibitisha tarehe halisi. Wachambuzi wanaona kuwa, ingawa Korea ya kaskazini inatilia maanani sana mawasiliano ya njia ya New York, lakini nchi hiyo inasisitiza mtindo wake kujiamulia katika mambo ya kidiplomasia, kwa hiyo haiwezekani kwa Korea ya kaskazini kutangaza hadharani tarehe ya mazungumzo hayo kwa kupitia tu mawasiliano huko New York, lakini mawasiliano hayo yameonesha juhudi zake.
Baada ya mawasiliano hayo, Marekani imeziarifu nchi zinazohusika kuhusu mawasiliano hayo, pande mbalimbali zimeyasifu. Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bwana Wang Guangya alisema kuwa, China inafurahia mawasiliano kati ya pande hizo mbili na kutumai kuwa mazungumzo ya pande 6 yataanzishwa tena katika wiki kadhaa zijazo. Ofisa mmoja wa wizara ya mambo ya nje na biashara ya Korea ya kusini alisema kuwa, mawasiliano hayo yameondoa kwa kiasi fulani wasiwasi wa Marekani kuhusu mwelekeo wa viongozi wa Korea ya kaskazini juu ya Marekani.
Karibu mwaka mmoja utapita tangu kukwama kwa mazungumzo ya pande 6, hivyo jumuiya ya kimataifa inaimasrisha juhudi za usuluhishi. Walimwengu wanatarajia kuwa chini ya juhudi za pande mbalimbali zinazohusika, mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia ya peninsula ya Korea yataanzishwa siku chache zijazo.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-09
|