Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-09 16:22:57    
Bw. Guan Chenghua aeleza mpango wa utekelezaji wa watu wanaojitolea kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008

cri

Sherehe ya kuanzishwa kwa mradi wa watu wanaojitolea kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008 tarehe 5 ilifanyika hapa Beijing, mji mkuu wa China, hii imeonesha kuwa " mpango wa utekelezaji wa watu wa kujitolea kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008" umeanzishwa. Kiongozi wa ofisi ya uratibu wa mambo ya watu wanaojitolea kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya Beijing ambaye pia ni mwendeshaji mkuu wa umoja wa vijana wa Beijing Bw. Guan Chenghua alipohojiwa na mwandishi wa habari alijulisha mpango huo.

Bw. Guan alisema kuwa, idadi ya watu wanaojitolea kwa ajili ya michezo ya olimpiki ya mwaka 2008 itafikia elfu 70, na kuongeza watu wengine elfu 30 ambao watatoa huduma katika mashindano ya Olimpiki ya walemavu ya mwaka 2008, idadi ya jumla ya watu wanaojitolea itafikia laki moja.

Watu wanaojitolea kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya Beijing wengi wao watachaguliwa kutoka kwa wanafunzi laki 6 wanaosoma katika vyuo vikuu vya Beijing, na watu wengine wenye uwezo maalumu wanaojitolea wataandikishwa kutoka sehemu nyingine za China au nchi za nje. Watu wanaojitolea watatofautiana kwa aina 10 wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu, wanafunzi wa shule za sekondari, watu kutoka maeneno mbalimbali ya jamii, watu kutoka mikoa na miji mikubwa, watu kutoka " miji mitano ya mashindano ya Olimpiki", watu kutoka HongKong na Macao, wachina wanaoishi katika nchi za nje, wanafunzi wa kigeni wanaosoma mjini Beijing, watu wanaojitolea wa kimataifa na watu wanaofanya kazi maalum ya kujitolea.

Bw. Guan Chenghua alijulisha masharti ya kimsingi ya watu wanaojitolea wa mashindano ya olimpiki ya Beijing :

Hadi itakapofikia mwezi Aprili mwaka 2008 watu wenye umri usiopungua miaka 18; wanaofuata sheria ya China; wenye uwezo na sifa bora zinazotakiwa; wanaopenda kutoa huduma kwa kwa hiari kwa michezo ya olimpiki ya Beijing; na kukubali uongozi wa kamati ya maandalizi ya michezo ya olimpiki ya Beijing. Mbali na hayo watu wanaojitolea wanapaswa kuwa na uwezo wa kuongea kwa lugha za kigeni.

Kazi ya kuandikisha watu wanaojitolea itaanza katika mwezi Agosti mwaka 2006 na itamalizika mwezi Aprili mwaka 2008. Bw. Guan alisema kuwa, huduma za watu wanaojitolea wa michezo ya olimpiki ni uzoefu muhimu katika maisha. Kama baadhi ya watu wakiwa na fikra ya kuangalia mashindano au kukutana na wachezaji nyota kwa kutumia jina la " watu wanaojitolea" watakata tamaa. Kwa sababu kazi za watu wanaojitolea ni kimya, wao ni " mashujaa wasiojulikana". Katika kipindi cha michezo ya olimpiki ya Beijing ya mwaka 2008, kamati kuu ya mashindano ya olimpiki ya Beijing itatoa bima, sare na mambo mengine yakiwemo mawasiliano, na chakula. Watu wanaojitolea kutoka nchi za nje au sehemu nyingine za Beijing watajitoa fedha za kusafirisha na maisha mjini Beijing.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-09