Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-09 18:50:01    
Kufuatilia "eneo la kijani"

cri

Zamani, wagonjwa wa Ukimwi walikuwa wanaogopa kwenda nje ya hospitali kutokana na wasiwasi wa kutambuliwa na watu wanaowafahamu. Pia ni rahisi kwa wagonjwa hao kuambukizwa na magonjwa mengine, kwa kuwa uwezo wao wa kujikinga na magonjwa umepunguzwa.

Kutokana na hali hiyo, mwezi Julai mwaka 2004, hospitali ya magonjwa ya kuambukiza ya mji wa Linfen mkoani Shanxi, ilitumia yuan zaidi ya milioni 1.5 kujenga eneo la kijani na kuwahimishia wagonjwa wa Ukimwi kwenye eneo hilo.

 

Mpaka sasa, wagonjwa zaidi ya 80 wa Ukimwi wamehamishiwa kwenye eneo hilo. Wanatakiwa kulipa gharama za maisha tu. wengi wa wagonjwa hao wanatoka kwenye familia maskini, hivyo hospitali hiyo pia ilianzisha shamba dogo kwenye eneo hilo, ili jamaa wa wagonjwa hao waweze kupanda mimea. Aidha, eneo hilo pia lina sehemu ya matibabu na sehemu ya usimamizi. Kwenye sehemu ya matibabu, jumba la burudani linaweza kustawisha maisha ya wagonjwa na jamaa zao.

 

Mtoto mmoja wa kike wenye umri wa 9 ni mgonjwa mdogo kabisa kwenye eneo hilo. Jina lake ni Cuicui. Aliambukizwa ugonjwa huo kutoka mama yake kabla hajazaliwa. Kabla ya kuja kwenye eneo la kijani, hakuongea sana na alikuwa anaogopa kuonana na watu ambao hawafahamu. Miezi kadhaa baada ya kuja kwenye eneo hilo, ameondoa hofu yake, kwenye siku ya watoto duniani tarehe 1 mwezi Juni mwaka huu, hata alishiriki kwenye michezo ya kuimba na kucheza pamoja na marafiki zake wadogo waliokuja kumwona. Baada ya kupewa matibabu kwa miezi hiyo, hali ya ugonjwa wa mtoto huyo ilidhibitiwa na kuboreka zaidi.

Hivi sasa, watoto wanne wanaishi kwenye eneo hilo, wote waliambukizwa ugonjwa wa Ukimwi kutoka mama yao. Hivi sasa, mgonjwa mwingine ambaye alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi Bi. Jin Yunfeng anawafundisha watoto hao kusoma na hisabiti.

 

Mwalimu huyo ana umri wa miaka 30 na aliambukizwa ugonjwa wa Ukimwi kutokana na kupewa damu baada ya uzazi. Tangu ugonjwa huo ugunduliwe, aliacha kazi na kuwategemea jamaa zake kumsaidia. Mume wake pia ameambukizwa ugonjwa huo, lakini bado anafanya kazi na kuwalea watoto wao. Bi. Jin Yunfeng alisema kuwa, kabla ya hapo, baadhi ya hospitali hata hazitaki kuwapokea wagonjwa wa Ukimwi. Lakini hivi sasa, hata wazazi wake waliokuja kumwangalia wote wamepata kazi kwenye eneo hilo.

Kwenye shajara ya Bi. Jin Yunfeng, aliandika kuwa, "nashukuru chama na serikali kutuangalia na kututunza, nashukuru viongozi wa hospitali hiyo kujenga nyumba hii nzuri kwa wagonjwa kama mimi, na kushukuru madaktari hodari wa hospitali hiyo kututibu na kutuokoa, na tunahisi upendo kila mahali, hatuhisi tena kuonewa wala kuwa wapweke tena."

Hali ya Bi. Jin Yunfeng si nzuri sana. Lakini alisema kuwa kuishi siku moja, atafurahia siku moja."

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-09