Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-10 19:03:23    
Kwa mara ya kwanza Jumuiya ya NATO yashiriki kwenye kazi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika

cri

Mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa ulinzi wa jumuiya ya NATO ulifunguliwa tarehe 9 huko Brussels. Azimio kuhusu kutoa uungaji mkono haraka kwa kazi ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Afrika huko Darfur, Sudan lilitolewa kwenye mkutano huo. Katika siku zijazo askari wa NATO watafanya kazi barani Afrika kwa mara ya kwanza.

Kutokana na azimio hilo, jeshi la NATO halitashiriki moja kwa moja kwenye kazi ya kulinda amani huko Darfur, bali litavisafirisha vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika katika sehemu mbalimbali kwa ndege, na kutoa mafunzo kwa askari wa jeshi la Umoja wa Afrika.

Kuna askari wapatao 8500 wa kikosi cha msaada wa usalama cha kimataifa kinachoongozwa na NATO nchini Afghanistan. Hii ni mara ya kwanza kwa NATO kutoa uungaji mkono kwa kazi ya ulinzi wa amani huko Darfur na kushiriki kwenye kazi ya kulinda amani barani Afrika. Hivi sasa NATO haijadokeza ratiba yake. Habari zinasema kuwa mpango wa kuwapeleka askari kwa ndege utatekelezwa mwanzoni mwa mwezi Julai.

Hivi sasa kuna askari wapatao 2300 wa Umoja wa Afrika huko Darfur. Kutokana na hali ya huko kuwa mbaya zaidi, Umoja wa Afrika umeamua kuongeza idadi ya askari kuwa 7700 kabla ya mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu. Hivi sasa Rwanda imeahidi kuongeza batalioni 3 huko, Senegal na Nigeria zote zitaongeza batalioni 2, na Afrika ya Kusini itaongeza batalioni 1. Na Umoja wa Afrika umepanga kuongeza askari huko hadhi kufikia elfu 12 mwakani.

Kutokana na mwaliko wa Umoja wa Afrika, tarehe 23 mwezi uliopita mwakilishi mwandamizi anayeshughulikia mambo ya nje na usalama wa Umoja wa Ulaya Bw. Javier Solana alisema huko Brussles kuwa, Umoja wa Ulaya utatoa uungaji mkono wa huduma na usafirishaji kwa kazi ya ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika. Baraza la NATO tarehe 24 lilitoa uamuzi likikubali kutoa uungaji mkono wa kijeshi ukiwemo usafirishaji, mafunzo ya askari na kuinua uwezo wa utafiti wa habari wa kikosi cha kulinda usalama cha Umoja wa Afrika.

Mgogoro wa Darfur ulianza mwezi February mwaka 2003, mpaka sasa umesababisha vifo vya watu laki 1.8 na watu milioni 2 kukimbia makazi yao. Baada ya usuluhishi wa jumuiya ya kimataifa, serikali ya Sudan na jeshi la upinzani vilifanya maduru mengi ya mazungumzo ya amani, lakini bado havijapata maendeleo halisi kuhusu suala la kusimamisha mapambano.

Kuhusu kutoa uungaji mkono kwa kazi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika, pande mbalimbali za NATO zilikuwa maoni tofauti. Marekani ilipanga kuwa kazi ya kutoa uungaji mkono na maandalizi ya askari kwa Umoja wa Afrika itaongozwa na NATO. Lakini waziri wa ulinzi wa Ufaransa Bw. Michele Alliot-Marie alisema kuwa, Ufaransa kusafirisha kikosi cha kulinda amani kwa Umoja wa Afrika ni sehemu moja ya uugaji mkono wa Umoja wa Ulaya. Lengo la Ufaransa la kujitenga na Marekani ni wazi sana.

Ufaransa ni mtangulizi wa mchakato wa utandawazi wa Ulaya, na imesifiwa kuwa injini ya utandawazi wa Ulaya pamoja na Ujerumani. Rais Chirac aliwahi kusisitiza kwa mara nyingi kuwa, kama hakuna ulinzi wa Ulaya hakutakuwa na Ulaya. Lakini Marekani ina wasiwasi kubwa kuhusu Umoja wa Ulaya kuendeleza mpango wa usalama na ulinzi wa pamoja usiohusika na NATO, na kuona kuwa Umoja wa Ulaya utashindana na NATO na kupunguza athari ya Marekani huko Ulaya, na mwishoni kudhuru maslahi yake barani Ulaya. Ingawa kwenye mkutano wa mawaziri wa ulinzi uliofanyika tarehe 9, katibu mkuu wa NATO Bw. Jaap de Hoop Scheffer alisisitiza kuwa NATO na Umoja wa Ulaya hazishindani kwenye suala la kutoa uungaji mkono kwa kazi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika, lakini maoni ya Ufaransa katika suala hilo bila shaka yameonesha kuwa bado kuna maoni tofauti kuhusu suala la ulinzi wa Ulaya kati ya Marekani na Ulaya.

Baada ya majadiliano mawaziri wa nchi wanachama wa NATO walikubaliana. Umoja wa Ulaya na NATO vyote vitafanya kazi ya kuwasafirisha askari wa kulinda amani, Ufaransa itasafirisha kikosi cha kulinda amani cha Senegal kwa niaba ya Umoja wa Ulaya, na Marekani itasafirisha kikosi cha Rwanda kwa niaba ya NATO.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-10