Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-10 19:45:43    
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bwana Chirau Ali Mwakwere tarehe 8 afika Beijing kwa ziara ya siku 5 nchini China

cri
Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bwana Chirau Ali Mwakwere tarehe 8 alifika Beijing kwa ziara ya siku 5 nchini China kutokana na mwaliko wa waziri wa mambo ya nje wa China Bwana Li Zhaoxing. Siku hiyo Bwana Li Zhaoxing alikuwa na mazungumzo na Bwana Mwakwere, ambapo Bwana Li alisema kuwa serikali ya China inapenda kufanya juhudi pamoja na serikali ya Kenya katika kuimarisha uhusiano wa aina mpya wa kiwenzi ulio wa muda mrefu na utulivu, na kuwa na usawa na kunufaishana.

Tarehe 10 mwandishi wetu wa habari amepewa nafasi ya kumhoji waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bwana Mwekwere. Sasa tunawaletea mahojiano hayo:

Mwandishi: Mheshimiwa waziri wa mambo ya nje wa Kenya, kwanza tafadhali naomba uelezee hali kuhusu maendeleo ya uhusiano kati ya China na Kenya katika sekta mbalimbali.

Waziri: Uhusiano baina ya China na Kenya ni mzuri sana, ni uhusiano ambao una manufaa makubwa kwa wakenya na wachina. Sisi watu wa Kenya tumepata msaada wa kila aina kutoka nchi ya China, tumeridhika na msaada kama vile mambo ya afya, maendeleo katika sekta ya maji, maendeleo ya kutengeneza barabara na maendeleo kadha wa kadha ya ukulima, kwa hivyo uhusiano wetu ni mzuri na una manufaa makubwa kwa wakenya na wachina.

Mwandishi: Unaona kuna maendeleo gani yanayopatikana miaka ya hivi karibuni katika ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika, hasa baada ya kuanzishwa kwa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika?

Waziri: Baada ya kuanzishwa kwa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, China ilikata shauri, iliaumua kuwa wananchi wao wanaweza kutembelea nchi za kiafrika kwa sababu zina usalama na watalii wanaweza kwenda Afrika bila wasiwasi. Walichagua Kenya, yaani wachina wenyewe na serikali ya China yewenye iliwaambia wanachi wao kuwa wanaweza kutembelea Kenya bila wasiwasi, kwa sababu wamekubali kuwa nchi ya Kenya iko salama. Na watalii watakuwa wananufaika sana kuona mengi na kuwasiliana na wakenya wenyewe. Pia tunaweza kupata msaada kadha wa kadha,kwa mfano kwa upande wa mawasiliano, upande wa kupeleka umeme katika sehemu zetu kadha wa kadha vijijini, na pia kuboresha mji wa Nairobi ambao kwa hivi sasa unahitaji mambo mengi ya wananchi wa Nairobi kuwa bora zaidi na wale ambao wanakuja kufanya kazi hapo kupata manufaa kadha wa kadha ya kufanya kazi zao kuwa rahisi .

 


1  2