Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-10 16:35:22    
Ushirikiano wa Mpango wa Galileo kati ya China na Ulaya unaenda vema

cri

Mazungumzo ya viongozi wakuu kuhusu Mpango wa Galileo wa Kuongoza Njia kwa Setilaiti (Galileo Satellite Navigation Programe) yalifanyika Beijing tarehe 9. Wajumbe waliohudhuria mazungumzo wa China na Umoja wa Ulaya wote wanaridhika na ushirikiano wa mpango huo baada ya China kujiunga nao.

Mpango huo wa Galileo ulianzishwa mwaka 2002, ni mpango wa mkakati wa utafiti wa sayansi kwa lengo la kuanzisha mfumo wa kuongoza njia duniani kwa kutumia setilaiti (GPS). Mfumo huo unaundwa kwa setilati 30 zinazoizungukia dunia kwenye anga kilomita kwa elfu 24, na utaanza kutumika mwaka 2008.

China ilijiunga na mpango huo mnamo mwezi Oktoba mwaka 2003, ni nchi ya kwanza isiyo ya Umoja wa Ulaya katika mpango huo na imeahidi kutenga Euro milioni 200.

Katibu mtendaji wa mpango huo wa Umoja wa Ulaya Bw. Rainer Grohe tarehe 9 alikuja Beijing na ujumbe wake na kufanya mazungumzo na wenzake wa China kuhusu hatua ifuatayo ya ushirikiano wa mpango huo. Baada ya mazungumzo, kwenye mkutano na waandishi wa habari mkuu wa wajumbe wa China Bw. Zhang Guocheng alisema, "Lengo la mazungumzo ni kuratibu kazi za China katika mpango huo wa Galileo na kubainisha miradi ya China. Kwenye mazungumzo, mimi na Bw. Grohe sote tunaridhika na ushirikiano tokea China ijiunge na mpango huo."

Bw. Zhang aliongeza, mazungumzo yalihusika na mashirika ya China namna ya kupata idhini maalumu ya kushiriki kwenye mpango huo na namna ya kushirikiana kati ya mashirika ya China kushirikiana na mkandarasi wa mpango wa Galileo, na namna ya kutumia teknolojia ya China katika mpango huo. Alidokeza kuwa mwezi ujao China na Umoja wa Ulaya zitasaini makubaliano kuhusu matumizi ya teknolojia ya China kwenye mpango huo.

Bw. Grohe alifurahia ushirikiano wa upande wa China. Alisema, ingawa nchi nyingi zina hamu na mpango huo, lakini hadi sasa hakuna nchi hata moja na kutenga fedha nyingi na kutoa mchango mkubwa kama China.

Bw. Grohe alisema, kujiunga na mpango huo kwa China kumeonesha matumaini ya China kushirkiana na Umoja wa Ulaya katika siasa na teknolojia. Anaamini kuwa mashirika ya China hakika yatapata fursa nzuri ya biashara kutokana na China kujiunga na mpango huo, na anaona furaha kwa teknolojia ya anga ya China kutumika katika mpango huo. Alisema, "Nafahamu kwamba China ina nguvu kubwa ya teknolojia ya anga, kwa hiyo natarajia ushirkiano wenye ufanisi wa China."

Bw. Grohe alieleza mpango unavyoendelea hivi karibuni. Alidokeza kuwa hivi sasa kuna mashirika makubwa yanayogombea haki ya kuendesha mpango huo, Umoja wa Ulaya utachagua mkandarasi mmoja wa uendeshaji wa mpango huo; na mwishoni mwa mwaka huu Ulaya itarusha setilaiti mbili kwa ajili ya mpango huo na setilaiti hizo zote zimetengenezwa na Ulaya.

Bw. Grohe alisisitiza kuwa mpango huo utaendelea kuenezwa katika dunia nzima. Alisema hivi sasa Israel imeomba kujiunga na mpango huo, na nchi za India, Korea ya Kusini, Austalia, Brazil, Argentina, Moroco, Ukraini pia zimeonesha nia ya kujiunga na mpango huo.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-10