Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-10 19:07:35    
Bingwa Mzee aliyevuka karne tatu

cri

Msanii mkubwa Bwana Liu Haisu, ni mwanzilishi wa elimu ya uchoraji wa kisasa wa China, alizaliwa mwezi Machi, 1896, huko mjini Changzhou, mkoani Jiangsu. Bw. Liu alianza kujifunza uchoraji tangu alipokuwa mtoto na alionekana mwenye kipaji.

Alipotimiza umri wa miaka 16, Bw. Liu aliondoka nyumbani, na kufika mji wa Shanghai ambao ulikuwa mji mkubwa wa China. Wakati huo China ilikuwa katika vuguvugu la kujifunza mambo mapya kutoka kwa nchi za magharibi. Bw. Liu alipendelea sanaa ya uchoraji wa Kimagharibi, akijumuika na wenzake waliokuwa na nia sawa naye, walifungua Shule ya Uchoraji ya Shanghai. Lengo la shule hiyo lilikuwa ni kukuza sanaa yenye asili ya Mashariki na kutafiti mafumbo ya sanaa ya Magharibi.

Shule hii iliungwa mkono na mtaalamu Cai Yuanpei. Shule hii ilipigania kujenga hali ya kujiamini binafsi, kuheshimu maumbile na kupendekeza wavulana na wasichana wasome pamoja shuleni. Pendekezo la shule la kumchora mtu akiwa uchi lilishtua sana jamii, lilipingwa na kukashifiwa vikali na watu. Hata Liu mwenywe alikabiliwa na hatari ya kukamatwa na polisi.

Mwaka 1919, Bw. Liu alikwenda Japani kufanya uchunguzi kuhusu elimu ya sanaa. Katika miaka ya thelathini alitembelea Ulaya mara kadha, alifanya maonyesho ya michoro na kutoa mihadhara huko Ufaransa, Italia, Uswisi, Ubelgiji na Ujerumani. Alifahamiana na Pablo Picasso na Henri Matisse. Alipokuwa mzee, akiitikia mialiko alizitembelea tena baadhi ya nchi hizo. Katika maisha yake yote, alitunukiwa aina 30 za tuzo za hadhi ya kimataifa. Aliwahi kuwa mgeni wa Rais wa zamani wa Ufaransa, waziri mkuu wa zamani wa Nakasone Yasuhiro Japani na viongozi wengine wa serikali. Kwenye maadhimisho ya miaka 98 ya kuzaliwa kwake Bw. Liu alijitungia mwenyewe shairi lisemalo.

"kutembelea mabara matano kwa na kuvuka bahari nne,

Kuishi maisha marefu kwa karne tatu."

Shairi hilo ndicho kiwakilishi cha maisha yake na njia ya sanaa aliyopitia.

Bw. Liu ni bingwa wa kuchora picha na kuandika maandikio ya sanaa ya kichina. Alikaririwa akisema kwamba katika sanaa ya maandikio ya kichina, wasanii inawapasa waunganishe ustadi wa zamani na ule wa kisasa, ustadi wa zamani na ule wa nchini, wawe na moyo wa kuvumbua mambo mapya na kamwe wasifuate kikasuku kanuni kongwe. Zaidi ya hayo, Bw. Liu alikuwa bingwa wa kuandika maandiko ya kalamu. Picha yake ya mafuta na ya jadi ya Kichina imepewa sifa kubwa. Bw. Liu alipenda sana kuchora Mlima Huangshan, aliwahi kupanda mlima huo mara 10 tangu apande kwa mara ya kwanza alipokuwa na miaka 22 hadi mara ya mwisho alipokuwa na miaka 92. picha ake nyingi zinaonyesha mandhari ya mawingu moshi yanayobadilikabadilika juu ya Mlima Huangshan. Picha yake ya mwisho ilikuwa ya mlima huo.

Kabla hajafariki, Bw. Liu alitoa kwa taifa picha zake zote za thamani na hazina alizohifadhi ili atimize tumaini lake la miaka mingi. Manispaa ya Shanghai ilijenga Jumba la Sanaa la Liu Haisu katika Wilaya ya Hongqiao, ambapo picha zake zinatunzwa vizuri kwa njia ya kisasa na kuoneshwa katika vipindi maalumu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-10