Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-13 10:59:42    
Tatizo la umaskini duniani haliwezi kutatuliwa kwa njia ya kusamehe madeni peke yake

cri
    Mawaziri wa mambo ya fedha wa kundi la nchi nane waliafikiana kwenye mkataba tarehe 11, kuondoa mara moja madeni ya dola za kimarekani bilioni 40 ya nchi 18 zilizo maskini kabisa duniani ili kupunguza tatizo la umaskini duniani. Huu ni mpango wa kwanza mkubwa duniani wa kusamehe madeni, hivyo umepongezwa na nchi husika. Lakini vyombo vya habari vinasema kuwa kutokomeza umaskini duniani kwa kutegemea kusamehe madeni bado hakutoshi, nchi zilizoendelea zingeongeza misaada ya maendeleo, kuondoa utoaji ruzuku na kufungua masoko kwa nchi maskini ili kuhuisha "uwezo wa kujiendeleza" wa nchi hizo.

    Nyingi wa nchi hizo 18 zinazosamehewa madeni ziko katika kusini mwa Sahara barani Afrika, kundi la nchi nane limekubali nchi hizo kutumia fedha za kulipia madeni katika kuendeleza elimu, matibabu, mambo ya afya na ujenzi wa miundo mbinu, hatua ambayo itapunguza shinikizo la fedha linalozikabili nchi hizo kwa kiwango fulani. Lakini nchi hizo ni dhaifu kutokana na matatizo ya miaka mingi ya maafa, maradhi na masuala mengi ya kijamii, fedha za madeni yanayosamehewa ni dola za kimarekani bilioni 40, na kila moja ya nchi hizo inapata wastani wa dola za kimarekani bilioni 2 tu, hivyo kimsingi haziwezi kuzitoa katika hali ya umaskini. Baadhi ya mashirika ya utoaji misaada duniani yamesema kuwa kwa nchi zinazoshindwa kurudisha fedha za madeni, kusamehewa madeni ni kufanya kazi ya kuondoa mzigo wa mawazo tu. Nchi zilizoendelea zingeongeza misaada ya maendeleo baada ya kusamehe madeni ya nchi hizo, kuondoa ruzuku ya kilimo na kufungua masoko kwa nchi hizo, lakini maoni ya nchi zilizoendelea kuhusu msimamo huo bado yanatofautiana sana.

    Katika upande wa kuongeza misaada ya maendeleo, ingawa Uingereza inaunga mkono kwa nguvu msimamo huo miongoni mwa kundi la nchi nane, lakini haiwezi kuafikiana na nchi nyingine 7. Kwa kufuata wazo hilo la Uingereza, nchi zilizoendelea zitatakiwa kutoa misaada maradufu ya maendeleo, ambayo itafikia dola za kimarekani bilioni 100 katika kipindi cha miaka 10 ijayo ili kufanya nchi hizo kuondokana na hali ya umaskini ya hivi sasa. Lakini Marekani haifurahishwi na wazo hilo la Uingereza. Hivi karibuni Marekani iliwahi kusema kuwa Marekani imekuwa mbele katika kuzisaidia nchi maskini za Afrika, na imekwishatoa misaada mingi. Mwanzoni mwa mwezi huu, waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair alitembelea Washington akitarajia nchi hiyo kubwa kabisa kiuchumi itakubali kutoa misaada mingi zaidi kwa upunguzaji umaskini duniani. Lakini rais Bush alitangaza kuwa itaongeza misaada ya dharura kwa dola za kimarekani milioni 674 tu kwa Afrika, kiasi ambacho ni kidogo sana kikilinganishwa na alichotarajia Bw. Tony Blair kutokana na msimamo wa Marekani, mkutano wa mawaziri wa nchi nane hata haukuweka suala la utoaji misaada katika ajenda za mkutano.

    Nchi zilizoendelea kuondoa ruzuku ya kilimo na kufungua masoko yao kwa nchi maskini imechukuliwa kuwa ni kuhuisha uwezo wa kujiendeleza wa nchi maskini, lakini si jambo rahisi kutokana na kila nchi ya nchi hizo infikiria maslahi yake yenyewe, si rahisi kwa Umoja wa Ulaya kurekebisha sera zake za kilimo cha pamoja katika kipindi cha karibuni.

    Hivi sasa kundi la nchi nane limepita hatua moja muhimu katika kuondoa madeni, sasa watu wanatarajia nchi hizo zitoa mchango mkubwa zaidi katika kuongeza misaada ya maendeleo na kufungua masoko. Ili kutimiza lengo lililowekwa na Umoja wa Mataifa kwa vitendo halisi.

Idhaa ya Kiswahili