Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-13 16:02:42    
Uwanja wa Tian An Men

cri

Beijing, mji mkuu wa China ni mji wenye historia ndefu, matukio mengi makubwa katika historia ya China yalitokea mjini Beijing, hivyo mjini Beijing yamejengwa majumba mengi ya makumbusho ya historia, Jengo jekundu la Chuo kikuu cha Beijing na Jengo la Mlango wa Tian An Men ni "mashahidi wawili maarufu wa historia", na tulizungumzia hali kuhusu Jengo jekundu la Chuo kikuu cha Beijing. Leo tunawaelezea kuhusu Jengo la Mlango wa Tian An Men wa Beijing.

Jengo la Mlango wa Tian An Men liko katikati ya mji wa Beijing na kando ya barabara la Changang. Hili ni jengo maarufu sana la Beijing, tarehe 1 Oktoba mwaka 1949, kwenye roshani ya uwanja wa Tian An Men, mwenyekiti Mao Zedong aliitangazia dunia nzima kuwa Jamhuri ya Watu wa China imezaliwa kuanzia siku hiyo.

Mlango wa Tian An Men mwanzoni uliitwa Mlango wa Cheng Tian Men, maana yake ni kuwa mlango huo ulifunguliwa na mungu na kumtii mungu, jengo hili lijengwa kuanzia enzi ya Ming ya mwanzoni mwa karne ya 15. Ilipofika wakati wa enzi ya Qing, mlango huo ulibadilishwa jina na kuwa Mlango wa Tian An Men, maana yake ni kumtii mungu na kuitawala nchi kwa usalama.

Jengo la Mlango wa Tian An Men wa wakati huo lilikuwa na uwanja mkubwa wenye hekta 11, pande zake za mashariki, magharibi na kusini zilikuwa kuta nyekundu, jengo hilo lilizungukwa kuwa sehemu iliyokuwa haiwaruhusu raia wa kawaida kuingia ndani. Jengo la Mlango wa Tian An Men lina kimo cha mita 34, vigae vyake vya fahari vya Liuli vyenye rangi ya dhahabu vinameremeta chini ya mwangaza wa jua ambavyo vinaonesha heshima na taadhima ya ufalme. Katika enzi ya Qing, sherehe kubwa za kutangaza amri au matangazo muhimu ya wafalme zilifanyika katika jengo hilo. Kutokana na kuwa sherehe kubwa ya kutangaza kuzaliwa kwa Jamhuri ya watu wa China ilifanyika katika uwanja wa Tian An Men mwaka 1949, Mlango wa Tian An Men umekuwa alama moja ya China mpya. Baadaye jengo la mlango huo lilifanyiwa ukarabati mara 4, sura yake imekuwa mpya kabisa, na uwanja wa Tian An Men umekuwa mahali muhimu pa kufanyia sherehe za shangwe au mikutano ya hadhara nchini China.

Kupanda roshani ya Jengo la Mlango wa Tian An Men, uwanja mkubwa zaidi kuliko nyingine duniani unaonekana wazi kwenye upeo wa macho ya watu. Watalii wanaweza kuona madaraja ya Jinshui chini ya roshani, pia wanaweza kutupia macho mbali majengo makubwa na marefu pembezoni mwa uwanja wa Tian An Men. Mtalii mmoja kutoka Italia aliyetembea kwenye roshani ya Jengo la Mlango wa Tian An Men Bwana Sophily alisifu sana mandhari nzuri ya sehemu ya jengo hilo akisema:

Uwanja wa Tian An Men ni mkubwa na mzuri sana. Jengo la Mlango wa Tian An Men linapendeza kama kasri la mfalme. Jengo hilo limehifadhiwa vizuri mpaka sasa, hii inawavutia sana watu na kunipa picha kubwa nzuri.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-13