Tangu kuanza kutumika kwa fedha za Euro, tofauti ya kiwango cha ongezeko la uchumi kwenye nchi zinazotumia Euro na nchi ya Marekani imekuwa kubwa mwaka hadi mwaka. Kura za maoni zilizopigwa hivi karibuni katika Ufaransa na Uholanzi zinaonesha kuwa, watu wa nchi hizo wanasusia "Mkataba ya Katiba ya Umoja wa Ulaya", hatua ambayo imefanya azma ya Ulaya kuelekea kwenye umoja wa kisiasa kuzuiliwa, ambapo msingi wa umoja wa sarafu umetingishwa, hata kuna baadhi ya maofisa wa vyeo vya juu nchini Italia, ambao wanasema kuwa ni afadhari waendelee kutumia sarafu zao za hapo zamani.
Katika muda wa miaka 6 na nusu tangu kuanza kutumika kwa Euro, kila mara wanapotokea watu kukosa imani juu ya Euro, serikali za nchi mbalimbali zinazotumia Euro na kamati ya Ulaya hutoa taarifa kueleza kuunga mkono kithabiti umoja wa sarafu. Mwanauchumi wa kwanza wa benki kuu ya Ulaya Bw. Otema Yisin hata alionya nchi hizo kuwa kujitoa katika umoja wa sarafu ni sawasawa na "kujiua".
Lakini hivi sasa idadi ya watu wenye mashaka juu ya Euro inaongezeka siku hadi siku.
Profesa wa chuo kikuu cha Luwen nchini Ubelgiji Bw. Paul Grofor alisema kuwa, umoja wa sarafu hauwezi kuwa imara ila tu kuungwa mkono na umoja wa kisiasa. Kuna watu wengi barani Ulaya wenye maoni ya namna hiyo. Wanaona kuwa elimu ya uchumi inasema kuwa, utulivu wa umoja wa sarafu kwa kawaida unahitaji kuwepo sera kuu za udhibiti kukabiliana na migogoro na changamoto mbalimbali. Kutokana na uzoefu wa siku zizolizopita, umoja wa sarafu utashindwa hatimaye ukiachana na umoja wa kisiasa. Hivi sasa katiba inayohimiza umoja wa kisiasa inasusiwa na nchi mbili za Ufaransa na Uholanzi, hivyo mustakabali wa umoja wa kisiasa umebadilika kuwa kitu kisichotegemeka. Ngozi ikiondolewa, manyoya yaliyoko kwenye ngozi yatakaa wapi? Endapo umoja wa kisiasa utashindwa hatimaye, basi umoja wa sarafu utaweza kuendelea kuweko?
Lakini kuna wanasiasa na wanauchumi wengi wanaona kuwa umoja wa sarafu utaweza kuendelea vivyo hivyo baada ya kuvunjika kwa umoja wa kisiasa. Bw. Yisin tarehe 3 mwezi huu alisema kuwa umoja wa sarafu utaweza kuendelea vizuri hata kukosa umoja wa kisiasa. Kamati ya Ulaya pia inaona hivyo, sababu ni kuwa kama kuna udhibiti mzuri wa mambo ya fedha, Benki Kuu huru na soko na nguvukazi lenye unyumbufu, umoja wa sarafu utaweza kuendelea bila wasiwasi.
Lakini kuna wataalam waliofanya uchambuzi kuwa mazingira ya kuweko kwa kamati ya Ulaya yamehatarishwa. Kwanza, udhibiti wa mambo ya fedha ni kama hakuna. "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko" unataka nchi 12 zinazotumia Euro kudhibiti nakisi kuwa chini ya 3% ya pato la nchi, lakini nchi kubwa zinazotumia Euro hazifuati agizo hilo, na kuonesha mfano mbaya kwa serikali za nchi mbalimbali kutodhibiti nakisi zake na kufanya mkataba huo kutokuwa na nguvu kwa serikali za nchi mbalimbali.
Pili, soko la nguvukazi bado halijaboreshwa. Kabla ya miaka mitano iliyopita wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya waliahidi huko Lisbon, mji mkuu wa Ureno kuwa wataendeleza kwa nguvu mageuzi ya uchumi, kuongeza unyumbufu wa masoko ya bidhaa na nguvukazi ili kukuza nguvu ya ushindani ya Ulaya duniani. Lakini hivi sasa ahadi zao zimekuwa maneno matupu.
Tatu, Sera za marekebisho ya sarafu za benki kuu ya Ulaya hazifanyi kazi sawasawa.
Umoja wa kisaisa umeokosa imani ya watu, mfumo wa udhibiti wa mambo ya fedha umeokosa nguvu, masoko ya nguvukazi yameyokosa unyumbufu, benki kuu iliyo kama kiwete na uchumi wa nchi kubwa unaozorota, vimefanya Euro kukosa imani ya watu.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-14
|