Tarehe 11 mkutano wa mawaziri wa fedha wa kundi la nchi 8 uliamua kuondoa madeni yenye thamani ya Dola za kimarekani bilioni 40 kwa nchi 18 masikini, nchi mbalimbali za Afrika zilipokaribisha uamuzi huo pia zilizitaka nchi za Magharibi ziondoe vizuizi vya biashara, na kufungua soko kwa bidhaa za Afrika, ili kuiwezesha Afrika kupata nguvu ya kujiendeleza kiuchumi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni Rais wa Nigeria Bw. Olusegun Obasanjo alisema kuwa, ingawa kuondoa madeni ya nchi za Afrika kunasaidia uchumi wa Afrika, lakini hakuisaidii Afrika kutimiza lengo la maendeleo ya Mileniam. Katika mkutano huo, kwa ujumla nchi 14 za Afrika zimeondolewa madeni, zikiwemo Uganda. Mshauri mwandalizi wa mambo ya habari wa Rais wa Uganda Bw. Nagenda alisema kuwa, nchi zilizoendelea zina desturi ya " kutoa msaruzuku kwa mkono mmoja na kurudisha msaruzuku huo kwa mkono mwingine". Kama nchi za Magharibi hazitaondoa vizuizi vya biashara kwa nchi masikini, ni vigumu sana kwa nchi za Afrika kuendeleza uchumi kwa kujitegemea.
Rais John Kuffor wa Ghana alisema kuwa, kama nchi zilizoendelea hazitaondoa sera ya kutoa ruzuku ya kilimo na vizuizi mbalimbali, haki ya uchumi wa nchi zinazoendelea itaharibika. Alisema kuwa, ingawa utoaji wa mazao ya kilimo ya Afrika uliongezeka kutokana na msaada wa mitaji ya kimataifa, lakini bidhaa za Afrika bado haziwezi kuingia kwenye soko la nchi zilizoendelea.
Afrika Kusini ilipokaribisha azimio ya kuondoa madeni, pia iliilaani sera ya kutoa ruzuku ya kilimo ya nchi za magharibi. Msemaji wa Rais wa Afrika Kusini alisema kuwa, kutatua suala la madeni kunahitaji juhudi kubwa zaidi.
Madeni ya nchi za Afrika ya mwaka 2005 yanakadiri wa kufikia dola za kimarekani bilioni 28.4. lakini idadi ya madeni yaliyoondolewa ni asilimia 14 tu. Kutokana na takwimu za Umoja wa Mataifa, kila mwaka, kiasi cha nchi za Afrika kulipa madeni kinafikia dola za kimarekani bilioni 23, ambayo inachukua asilimia 31 katika mapato ta fedha za kigeni. Hivi sasa, madeni ya nchi za Afrika yanaongezeka kwa 23% kila mwaka, miongoni mwa nchi 38 zenye madeni makubwa, nchi 32 ni za Afrika, na nchi hizo nyingi ni ndogo ambazo hazina nguvu ya kulipa madeni hayo.
Vyombo vya habari vya Afrika vinasema kuwa, kiasi cha kuondoa madeni ya Afrika hakiwezi kuisaidia Afrika kusukuma maendeleo ya uchumi wa Afrika, kuondoa umasikini barani Afrika kunapaswa ufunguaji mlango wa soko la kimataifa.
Mwaka 2002, ruzuku ya kilimo katika nchi zilizoendelea ilifikia dola za kimarekani bilioni 318, lakini nchi hizo zilitoa misaruzuku yenye thamani ya dola ya kimarekani bilioni 22 kwa Afrika. Kutokana na ruzuku kubwa ya kilimo ya Umoja wa Ulaya na Marekani, mwaka 2001, Mali ilipata hasara ya dola za kimarekani milioni 43 katika biashara ya pamba. sera ya ruzuku ya kilimo ya nchi za Magharibi iliwafukuza wakulima wa Afrika kwenye nje ya soko. Wakati huo huo, bidhaa za kilimo kutoka nchi za Magharibi zinakaribishwa sana duniani, bei ya bidhaa za kilimo katika soko la kimataifa bado ni mbaya.
Katika mkutano huo, mawaziri wa fedha wa kundi la nchi 8 walikataa Kenya na Nigeria nje ya msamaha wa madeni kwa sababu ya ufisadi, watu mashughuli walilaani kitendo hicho cha kuhusisha suala la uchumi na suala la siasa.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-14
|