Shirika la mafuta la kimataifa OPEC tarehe 15 litafanya mkutano wa 136 wa mawaziri wa nchi wanachama huko Vienna ili kujadili namna ya kupunguza bei ya mafuta duniani. Lakini vyombo vya habari vinaona kuwa mkutano huo utashindwa kufikia lengo hilo.
Tarehe 13 bei ya mafuta ya asili duniani kwa mara nyingine ilipanda zaidi kwa dola za Kimarekani 2.08 kwa pipa moja, na kufanya bei ya kila pipa kuwa dola za Kimarekani 55.62, ambayo ni rekodi mpya tokea tarehe 6 Aprili; bei ya mafuta yaliyoagizwa na kuyapata mwezi Julai mjini London ilipanda kwa dola za Kimarekani 2.11 kwa pipa na kufanya bei ya kila pipa kuwa dola za Kimarekani 54.78. Wachambuzi wanaona kuwa ingawa OPEC itaongeza uzalishaji mafuta, lakini kutokana na mahitaji makubwa duniani bei ya mafuta haitapungua.
Tokea mwezi Mei, bei ya mafuta imekuwa kubwa, na katikati ya mwezi huo iliwahi kupanda hadi kufikia dola za Kimarekani 56 kwa pipa moja, lakini katika mwezi wa Juni bei yake huwa kiasi cha dola za Kimarekani 53 hivi kwa pipa. Ingawa wiki iliyopita Bw. Ali al-Naimi, waziri wa madini na mafuta wa Saudi Arabia, nchi ambayo inazalisha mafuta kwa wingi kabisa duniani alisema kuwa OPEC inapaswa kuongeza mapipa laki 5 juu ya msingi wa mapipa milioni 27.5 kila siku, lakini kauli yake haikuleta athari yoyote sokoni. Wachambuzi wanaona kuwa hata kama kweli OPEC ikiamua kama alivyosema, bei ya mafuta ya asili haitaweza kupungua katika kipindi kifupi. Sababu ni zifuatazo:
Kwanza, ni shida kwa OPEC kuongeza zaidi uzalishaji mafuta. Hivi sasa nchi wanachama wa OPEC zimezidiwa uwezo wao wa kuzalisha mafuta, na nchi nyingi hazina uwezo zaidi. Waziri wa mafuta wa Iran, nchi ambayo ni ya pili kwa kuzalisha mafuta duniani Bw. Bijan Zanganeh tarehe 13 mjini Tehran alisema kuwa hivi sasa nchi wanachama wa OPEC hazina uwezo wa kuzalisha mafuta mengi zaidi na pia hazina uwezo wa kudhibiti bei ya mafuta. Kwa hiyo. Hali hiyo imedhihirisha kuwa ingawa OPEC inaendelea kudhibiti maliasili ya mafuta duniani, na hakuna shirika lolote lingine linaloweza kufanya kazi badala yake, lakini uwezo wake wa kudhibiti bei ya mafuta umedhoofika ikilinganishwa na zamani.
Pili, majira ya kimbunga cha tropiki kutoka Caribean yamefika na kimbunga kinaharibu sana muundombinu za uzalishaji mafuta katika Ghuba ya Mexico. Wiki iliyopita soko la mafuta liliathiriwa vibaya na kimbunga cha tropiki ya Caribean, ingawa sasa athari ya kimbunga hicho imepungua lakini idara ya utabiri wa hali ya hewa ya baharini nchini Marekani imetangaza kuwa, mwaka huu tokea mwezi Juni hadi Novemba kimbunga kitatokea mara nyingi kuliko miaka yote iliyopita. Kutokana na kuwa mwaka uliopita kimbunga cha tropili kiliharibu sana muundombinu ya uzalishaji mafuta, watu wanahofia kuwa mwaka huu utakuwa hivyo hivyo.
Tatu, mahitaji ya mafuta duniani yanaongezeka siku hadi siku. Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani lenye makao makuu mjini Paris tarehe 10 ilichapisha makadirio yake kwenye jarida la kila wiki la soko la mafuta duniani kwamba mwaka huu mahitaji ya mafuta kwa wastani kila siku yanaongezeka kwa 2.2% yaani mapipa milioni 1.78, mahitaji ya jumla duniani kwa siku ni mapipa milioni 84.31. Isitoshe, kutokana kuwa majira ya utalii yamefika katika kizio cha kaskazini cha dunia hasa nchi za Marekani na Ulaya, mahitaji ya mafuta yataongezeka kwa kiwango kikubwa.
Aidha, hali hiyo ikiwa ni pamoja na biashara ya magendo na hali ya wasiwasi nchini Iraq, bei ya mafuta duniani haitapungua kama inavyotarajiwa. Wachambuzi wanaona kuwa mkutano huo wa OPEC hautakuwa na mafanikio yoyote katika kupunguza bei ya mafuta.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-14
|