Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-15 16:47:39    
Mkutano wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya wakabiliwa na matatizo mawili magumu

cri

Viongozi wa nchi 25 wanachama wa Umoja wa Ulaya watafanya mkutano kati ya tarehe 16 hadi 17 mjini Brussels. Mkutano huo utakumbwa na matatizo magumu mawili: Moja ni katiba na nyingine ni bajeti.

Huu ni mkutano wa kawaida wa kila baada ya miaka minne. Lakini kutokana na Ufaransa na Uholanzi kukataa katiba ya Umoja huo kwenye kura za maoni, hatima ya katiba hiyo imekuwa mada kuu ya mkutano huo na kuufanya mkutano huo kuwa usiwe wa kawaida.

Katiba ya Umoja wa Ulaya ni katiba ya kwanza ya Umoja huo, na inachukuliwa kama ni kumbukumbu muhimu katika mchakato wa ukamilifu wa Umoja huo. Mwezi Oktoba mwaka jana viongozi wa nchi wanachama walisaini katiba hiyo mjini Roma, kutokana na mpango, nchi wanachama zitamaliza taratibu za kuidhinisha katiba hiyo kabla ya mwezi Novemba mwaka 2006. Lakini Ufaransa na Uholanzi zilikataa katiba hiyo kwenye kura za maoni katika miezi ya Mei na Juni, na baadaye Uingereza iliacha kutimiza taratibu za kuidhinisha katiba hiyo. Matukio hayo ni pigo na ni tishio kwa hatima ya katiba hiyo.

Ili kukabiliana na tishio hilo, mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya, waziri mkuu wa Luxembourg Bw. Jeanp Claude Juncker kwa nyakati tofauti alizungumza na viongozi wa Ufaransa, Ujerumani na Italia akijaribu kusuluhisha misimamo tofauti ili katiba hiyo iamuliwe kabla ya mkutano huo wa viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya.

Kwa mujibu wa hali ilivyo sasa, ingawa katiba hiyo ilikataliwa nchini Uholanzi na Ufaransa, lakini viongozi wakiwemo viongozi wa nchi hizo mbili wote wanatetea kuwa taratibu za kuidhinisha katiba hiyo lazima ziendelee, na haifai kutangazwa kuwa katiba hiyo imekwisha kufa. Matatizo yaliyotokea katika mchakato wa kuidhinisha katiba hiyo pengine yatakuwa mjadala muhimu kati ya viongozi, yaani, kasi ya mchakato wa ukamilifu wa Umoja wa Ulaya itapungua au la, upanuzi wa Umoja huo utaathiriwa na namna ya kuwafahamisha watu wa Ulaya katiba hiyo na kuwafanya waiunge mkono.

Licha ya katiba ya Ulaya, bajeti ya kipindi cha tokea mwaka 2007 hadi 2013 ni mada nyingine muhimu katika mkutano huo. Ili bajeti hiyo iweze kupata makubaliano, mawaziri wa nchi za Umoja wa Ulaya siku za karibuni walifanya mikutano mara kadhaa, na mawaziri wa mambo ya nje pia walifanya mikutano ya faraghani mara kadhaa. Lakini kwa sababu kila nchi inashikilia msimamo wake hawakukubaliana kabla ya mkutano huo utakaoanza tarehe 16.

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zinahitilafiana katika matatizo mawili: Moja ni kuwa kamati ya Umoja wa Ulaya inaona kuwa fedha zilizochangwa na kila nchi mwanachama zisiwe chini ya 1.14% ya mapato ya taifa, hivyo ndivyo inavyoweza kuhakikisha vyombo vya Umoja huo vinafanya kazi kama kawaida na kukamilisha malengo ya fani mbalimbali za Umoja huo. Lakini Austria, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Uholanzi, nchi ambazo 1.14% ya mapato ni kubwa kuliko ruzuku zinazozipata kutoka Umoja huo zinataka kiasi hicho kipungue hadi 1%. Luxembourg imetoa msimamo wa katikati, lakini msimamo huo haujakubaliwa na pande zote.

Pili ni tatizo la fedha zilizorudishwa kutoka kwenye bajeti. Kuanzia mwaka 1984, Uingereza kila mwaka inaweza kupata fedha zilizorudishwa kutoka bajeti ya Umoja wa Ulaya dola za Kimarekani bilioni kadhaa, ni nchi pekee inayopata fursa nafuu hiyo. Lakini kutokana na mabadiliko ya Uingereza na nchi nyingine za Umoja huo, nchi nyingi wanachama zimekuwa na malalamiko makubwa. Hivi sasa nchi wanachama zinataka Uingereza iache fursa hiyo au kutunga kanuni zenye usawa kwa nchi zote wanachama. Lakini serikali ya Uingereza mara nyingi inatangaza kuwa hakuna uwezekano wa kujadili swala hilo, kwa sababu fursa hiyo Uingereza inaipata kutokana na kuwa ruzuku inayopata kutoka Umoja wa Ulaya ni ndogo.

Kwa sababu bajeti hiyo inahusika moja kwa moja na mpango utakaotekelezwa na hata inahusiana na vyombo vya Umoja wa Ulaya kuweza kuendelea na kazi kwa kawaida. Viongozi watajitahidi kukubaliana, lakini kila upande utasikiliza vipi na upande mwingine, jibu litapatikana baadaye.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-15