Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-15 19:18:09    
Mapishi ya vipande vya nyama ya kondoo na vitunguu maji

cri

Mahitaji

Nyama ya paja la kondoo gramu 200, vitunguu maji gramu 200, mchuzi wa soya gramu 50, mvinyo wa kupikia gramu 20, mafuta gramu 50, kiasi kidogo cha vitunguu saumu, pilipili manga, chumvi, siki, wanga na mafuta ya ufuta.

Njia

1. Ikate nyama ya paja la kondoo iwe vipande, na vipakue ndani ya bakuli moja, tia mafuta, mchuzi wa soya, chumvi, mvinyo wa kupikia na pilipili manga na wanga korogakoroga. Pia uvikate vitunguu maji na vitunguu saumu viwe vipande vipande.

2. tia mafuta ndani ya sufuria, pasha moto mpaka iwe nyuzi ya asilimia 60, tia vitunguu saumu ndani ya sufuria, koroga koroga halafu tia vipande vya nyama ya kondoo, korogakoroga kwa haraka, tia vipande vya vitunguu maji na chumvi koroga kwa haraka, mwisho mimina siki na mafuta ya ufuta. Vipakue, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.