Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-15 20:24:25    
China yaimarisha zaidi kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi

cri

Baraza la serikali la China tarehe 15 limeitisha mkutano na kuamua kuimarisha zaidi kazi ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi.

Mkutano huo umeamua kuwa, kuiweka kazi ya kinga na tiba ya ukimwi kwenye mpango wa maendeleo ya nchi, ikiwa kazi kubwa ya afya ya umma, na fedha za matumizi zitatolewa kwenye bajeti ya fedha; kuimarisha zaidi uenzi wa ujuzi wa kinga na tiba ya ukimwi kwa raia wote, kuimarisha kazi ya ufuatiliaji wa maambukizi ya ugonjwa na kukamilisha mfumo wa ufuatiliaji; kutekeleza hatua mbalimbali za kuwaokoa, kuwatibu na kuwafuatilia wagonjwa wa ukimwi na kuhakikisha haki na maslahi yao halali; kuimarisha utafiti wa kisayansi kuhusu kinga na tiba ya ukimwi na kuharakisha utengenezaji wa chanjo na dawa zinazohusika ili kupata njia zenye mafanikio za kutibu ugonjwa wa ukimwi.