Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-16 15:54:49    
Kusikilizwa kwa kesi ya Sadaam Hussein kwakabiliwa na shida nyingi

cri

Mahakama maalum ya Iraq tarehe 15 ilitoa hadharani kaseti ya video kuhusu kusikiliza mashtaka ya kesi za ndugu ya Saddam Hussein na maofisa wawili waandamizi wa utawala wa Saddam. Mahakama hiyo ilieleza katika taarifa yake kuwa kusikiliza mashtaka kulikofanywa tarehe 13, ni kwa ajili ya kuchunguza makosa yaliyofanywa na watu hao watatu katika miaka ya 80 ya karne iliyopita na mwaka 1991 dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shiah walioko kusini mwa Iraq na Wakurd walioko kaskazini mwa nchi hiyo.

Hii ni mara ya pili kutoa hadharani kaseti ya video kwa mahakama maalum ya Iraq ndani ya siku tatu kuhusu kusikiliza mashtaka ya Saddam na wafuasi wake, jambo ambalo limeonesha kuwa kazi ya kusikiliza mashtaka ya kesi ya Saddam bado inaendelea. Lakini watu wanaojua mambo halisi wanaona kuwa mnamo miezi 18 iliyopita tangu Saddam alipokamatwa, kazi ya kusikiliza mashtaka yake ilifanywa kwa taabu sana.

Hali ya usalama ya nchini Iraq haijabadilika mpaka hivi sasa. Tangu tarehe 28 mwezi Aprili serikali ya mpito ya Iraq ilipoundwa, watu karibu mia 900 wamekufa katika mashambulizi mfululizo. Tangu mwezi Machi mwaka 2003, vita vya Iraq vilipoanzishwa, idadi ya vifo vya askari wa Marekani walioko nchini Iraq imezidi 1700. Utawala wa Iraq unataka kusikiliza mashtaka ya Saddam na kuthibitisha makosa yake haraka iwezekanavyo na kupambana na ari ya wafuasi wa Saddam na Waislam wa dhehebu la Suni. Msemaji wa serikali ya mpito ya Iraq Bw. Laith Kuba tarehe 5 alisema kuwa serikali hiyo inataka kusikiliza mashtaka na kutoa hukumu haraka na kupunguza idadi kubwa ya mashtaka ya Saddam. Waziri mkuu Ibrahim Al-Jaafari alieleza faraghani kuwa kama mahakama itamkuta Saddam na hatia, huenda atapewa adhabu ya kifo.

Lakini mahakama hiyo tarehe 7 ilitoa taarifa kuwa, hadi sasa bado haijathibitisha tarehe ya kusikiliza mashtaka ya Saddam.

Kucheleweshwa mara kwa mara kwa kusikiliza mashtaka ya Saddam kuna sababu zifuatazo.

Kwanza, mahakama hiyo inataka kusikiliza mashtaka ya maofisa waandamizi wa utawala wa Saddam, halafu itasikiliza mashtaka ya Saddam, kwani maofisa hao yumkini watatoa ushahidi kuhusu makosa ya Saddam ili kusamehewa makosa yao na kusaidia kuthibitisha makosa ya Saddam.

Pili, kazi za maandalizi ya kusikiliza mashtaka ya Saddam ni nyingi sana na zinahitaji muda wa miaka miwili.

Mbali na upande wa mashtaka, upande wa utetezi wa Saddam pia unaharakisha kazi zao. Kikundi cha mawakili wanaomtetea Saddam kilichoko mjini Amman, Jordan kilikosoa ofisa wa serikali ya mpito ya Iraq kutoa mashtaka ya Saddam, kuingilia kazi za kusikiliza mashtaka na kunyima uhalali wa mahakama maalum. Kwa hiyo, namna ya kutenda mashtaka kiliyotoa kikundi hicho cha mawakili, hizo pia ni taabu zinazokabili kazi ya kusikiliza hukumu ya Saddam.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-16