Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-17 20:07:06    
Mvulana kutoka Tanzania anayejifunza sarakasi huko Wuqiao nchini China

cri
    Siku hizi, ngoma moja yenye mtindo wa kiafrika inavuma mara kwa mara hivi karibuni katika bweni la wanafunzi wa nchi za nje wanaosoma katika Shule ya Sarakasi ya Wu Qiao ya China. Mpiga ngoma ni mvulana kutoka Tanzania anayeitwa Godfrey Mwaipungu, rafiki zake waChina humwita Gao Fei. Gao Fei anayejifunza sarakasi huko Wuqiao, anaishi vizuri nchini China chini ya matunzo ya walimu na wanafunzi wa China.

    Wilaya ya Wuqiao iko katika mkoa wa Hebei ulioko karibu na Beijing, ambapo ni chimbuko la sarakasi ya China, na iliendesha awamu 9 za Sikukuu ya kimataifa ya Sarakasi ya Wuqiao ya Kimataifa ya China, na jina la "Wu Qiao" linajulikana zaidi nchini China na nchi za nje kutokana na sarakasi. Shule ya Sarakasi ya Wuqiao ya Hebei ni shule inayowaandaa wachezaji wa sarakasi, ambayo ina wapo wanafunzi wa China, na wanaotoka nchi za nje.

    Hivi sasa Shule ya sarakasi ya Wu Qiao imewaandaa wanafunzi zaidi ya 30 kutoka nchi za nje zikiwemo za barani Asia, Ulaya, Marekani na Afrika. Tulipokutana na Godfrey mwaipungu yaani Gao Fei kwenye ukumbi wa mazoezi ya wanafunzi wa shule ya sarakasi, alikuwa akifanya mazoezi ya kuvaa kofia ambayo ni mchezo mmoja wa sarakasi, pamoja na wenzake watatu. Ingawa amefika China kwa miezi minne tu, lakini aliweza kuongea nasi kwa kichina.

    "Mimi naitwa Gao Fei. Nina umri wa miaka 19. Naipenda China, pia napenda sarakasi ya China."

    Mwishoni mwa mwezi Septemba, mwaka 2004, Gao Fei na watoto wengine 17 wa Afrika walikwenda huko Wuqiao. Kati ya watoto hao, mwenye umri mkubwa zaidi ana miaka 20, mdogo kabisa ana umri wa miaka 12 tu. Wanafunzi hao 18 kutoka nchi za nje watasoma nchini China kwa mwaka mmoja, na watafanya maonesho hapa Beijing mwezi Oktoba mwaka huu. Hii ni kazi kubwa kwa wanafunzi na walimu wao.

    Shule hiyo ilimwandalia Gao Fei michezo kadhaa ikiwemo ustadi wa kuchezea kofia, baiskeli na Wu Shu. Kocha wake Chen Shujun alimwambia mwandishi wa habari kuwa, Gao Fei ni mwanafunzi mwenye bidii. Mara kwa mara anafanya mazoezi katika muda wa mapumziko. Sasa amepata maendeleo makubwa zaidi.

    " Hivi sasa Gao Fei anafanya mazoezi kwa bidii, na kupata maendeleo makubwa katika pande zote zikiwemo nguvu na vitendo."

    Gao Fei ni mchezaji wa Kundi la dansi nchini Tanzania, lakini bado ni ngumu kwake kujifunza sarakasi. Hivyo, maendeleo yake makubwa yanatokana na juhudi zake kubwa.

    Kila asubuhi, yeye ni mtu wa kwanza kufanya mazoezi ya mwili katika ukumbi wa mazoezi. Na kila ifikapo mwishoni mwa wikiendi, wakati wanafunzi wengine wanapopumzika, Gao Fei hufanya mazoezi kwa makini kama kawaida. Wakati wa mazoezi, Gao Fei alifahamiana na marafiki wengi wa China, Xu Mingming ni rafiki yake mzuri. Akisema:

    "Sisi ni marafiki wazuri, ninamweleza makosa yake wakati anapofanya mazoezi. Yeye pia hunitembelea ninapofanya mazoezi ya ustadi mpya."

    Chini ya misaada ya makocha na marafiki wa China, Gao Fei amepata ustadi mwingi zaidi wa sarakasi, wakati huo huo, anapenda zaidi sanaa ya sarakasi ya China. Alisema kuwa, michezo ya sarakasi ya China ni ya aina mbalimbali, na amepania kuonesha ustadi huo kwa waafrika wote baada ya kurudi nchini Tanzania. Akisema:

    " Hivi sasa nimecheza vizuri katika michezo kadha wa kadha kama vile ustadi kuchezea kofia na vichekesho. Baada ya kurudi nchini Tanzania, nitaanzisha kikundi cha sarakasi, na kuongoza kikundi hicho kufanya maonesho barani Afrika."

    Mwezi Desemba mwaka 2004, wanafunzi 12 kutoka Afrika wa Shule ya saNaa ya Sarakasi ya Wu Qiao walikwenda Ethiopia kufanya maonesho ya michezo ya sarakasi. Wakati huo, Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao aliyehudhuria kwenye Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika pamoja na viongozi zaidi ya 30 wa Afrika walitazama maonesho hayo nchini humo. Maonesho hayo mazuri sana yalisifiwa na viongozi wa China na Afrika na watazamaji wote.

    Ingawa Gao Fei hakushiriki kwenye maonesho hayo ya mchezo, lakini mafanikio waliyopata wenzake yamekuwa nguvu ya kumhimiza Gao Fei kupiga hatua katika njia ya kusonga mbele. Wanatarajia kuonesha ustadi wa sarakasi za China nchini kwao katika siku za baadaye.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-17