Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-17 22:06:50    
Umoja wa Mataifa watoa taarifa ikisema kuwa eneo la jangwa duniani kote linapanuka

cri

Umoja wa Mataifa tarehe 16 ulitoa taarifa ikisema kuwa, hali ya hewa inayobadilika kuwa joto imesababisha asilimia 41 ya ardhi ya ukame kote duniani inavia siku hadi siku, na eneo la jangwa kote duniani linapanuka siku hadi siku, na idadi kubwa ya watu watakabiliwa na matatizo ya maisha.

Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa, taarifa hiyo ya Umoja wa Mataifa imedhihirisha kuwa, sehemu zenye ukame ni sehemu zote zenye ardhi ya ukame ya nusu unyevunyevu hadi ardhi yenye ukame kabisa. Mashamba ya sehemu ya mashariki ya bahari ya Mediterranean ni mfano wa ardhi ya ukame ya nusu unyevunyevu, na jangwa la Sahara ni ardhi yenye ukame kabisa. Matokeo ya utafiti yameonesha kuwa, hivi sasa asilimia 10 hadi 20 ya ardhi za sehemu zenye ukame zinazowalisha idadi ya watu bilioni 2.1 duniani zimekuwa haziwezi kulimwa tena, na kupoteza thamani ya kiuchumi. Taarifa hiyo imeainisha kuwa, katika miaka 30 ijayo, idadi kubwa ya watu wanaoishi hivi sasa katika sehemu hizo watakabiliwa na shinikizo la kutafuta maskani mapya na kubadilisha njia yao ya maisha.

Taarifa hiyo imedhihirisha kuwa, hivi sasa watu wa sekta ya sayansi hawana uelewa juu ya namna jangwa kubwa linavyoumbika na linavyobadilikabadilika. Lakini hali ya mambo inayoonekana wazi ni kuwa, eneo la jangwa la duniani kote linapanuka siku hadi siku, hali ya jangwa kwenye ardhi imekuwa tatizo kubwa linaloleta athari kubwa mbaya kwa idadi kubwa ya watu duniani. Kimbunga cha mchanga kilichoumbika kwenye jangwa la barani Asia na Afrika hata kimeathiri afya ya idadi ya watu wa Amerika ya kaskazini. Tatizo kubwa na baya zaidi linaloletwa na hali ya jangwa kwenye ardhi ni kuwa mashamba hayawezi kulimwa tena, na kusababisha watu maskini wa sehemu zenye ukame kutoweza kuzalisha mazao na kujiendeleza.

Taarifa hiyo ya Umoja wa Mataifa imeainisha mwishoni kuwa, kila nchi inapaswa kuchukua hatua mwafaka kutokana na hali halisi ya nchi hiyo katika kutatua matatizo yanayosababishwa na hali ya jangwa kwenye ardhi. Njia zenye ufanisi zikiwemo kuwekeza vitega uchumi katika sehemu zenye ukame, kuanzisha shughuli za kuanzisha utalii wa kiviumbe, kuendeleza nishati ya jua, kuacha kilimo na kuanzisha shughuli za uvuvi. Hizo zote ni njia ya kutumia nishati finyu ya maji kwa kujipatia faida kubwa za kiuchumi.

Taarifa hiyo ni matokeo ya utafiti wa Umoja wa Mataifa juu ya hali ya jangwa kwenye ardhi katika mradi wa "kutathimini mfumo wa viumbe wa milenia". Taarifa hiyo imetolewa katika maadhimisho ya siku ya 11 ya "dunia kukinga na kushughulikia hali ya jangwa na ukame". Tarehe 17 Mwezi Juni mwaka 1994, nchi 191 zilisaini mkataba katika Umoja wa Mataifa zikipania kutatua tatizo la kupanuka kwa jangwa .

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-17