Tarehe 16 usiku, waziri mkuu wa Luxemburg, nchi mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya Bwana Jean Claude Juncker alitangaza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya siku hiyo kwenye mkutano wa wakuu walikubali kuahirisha kikomo cha siku ya kuidhinisha "Mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya" kwa nchi wanachama mbalimbali. Wachambuzi wanaona kuwa, hili ni chaguo pekee lenye busara la viongozi wa Umoja wa Ulaya.
"Mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya" ni mkataba wa kwanza wa katiba wa Umoja wa Ulaya, na ni mnara muhimu wa mchakato wa utandawazi wa Umoja, kazi yake ni kuhakikisha Umoja wa Ulaya uliopanuliwa unaweza kuendeshwa kwa ufanisi. Kutokana na mpango uliowekwa, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zinapaswa kukamilisha utaratibu wa kuidhinisha mkataba huo kabla ya mwezi Novemba mwaka 2006, ili mkataba huo ufanye kazi rasmi. Lakini siku chache zilizopita, Ufaransa na Uholanzi zilikataa mkataba huo katika upigaji wao wa kura za raia, hatua hii imeufanya mustakbali wa mkataba huo uwe tatizo lenye taabu linalowakabili viongozi wa Umoja wa Ulaya. Viongozi wa Umoja wa Ulaya tarehe 16 walijadili na kuamua kuahirisha kikomo cha kuidhinishwa kwa mkataba huo.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Bwana Juncker alisema kuwa, viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaona kuwa mkataba huo umetoa majibu sahihi juu ya maswali mengi yanayofuatiliwa na raia wa Ulaya, hivyo utaratibu wa kuidhinisha mkataba huo unatakiwa kuendelea kutekelezwa. Kutokana na Ufaransa na Uholanzi kukataa mkataba huo katika upigaji kura za maoni ya raia, Umoja wa Ulaya unatakiwa kujikosoa kwa muda fulani. Kuhusu suala la mkataba huo, katika siku zilizopita, Umoja wa Ulaya ulisisitiza tu mpango wa A, lakini haukuweka mpango wa B. Katika hali ya hivi sasa, Umoja wa Ulaya bado haujaweka mpango wa B, lakini viongozi wa Umoja wa Ulaya wameamua kubadilishana maoni kwa kupitia demokrasia, mazungumzo na majadiliano. Bwana Juncker alisisitiza kuwa, viongozi wa Umoja wa Ulaya wameona kwa kauli moja kuwa, Mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya haujafa, hakuna uwezekano kwa Umoja wa Ulaya kufanya majadiliano tena kuhusu mkataba huo. Hivi sasa Umoja wa Ulaya unatakiwa zaidi kuelewa zaidi maoni ya raia wa Ulaya, na kuwafahamisha kwa makini zaidi Mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya. Alisema, kuhusu kikomo cha siku ya kuidhinisha mkataba huo, huenda watajadili na kukitatua mwezi Januari hadi Julai wakati Austria itakapokuwa nchi mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya.
Vyombo vya habari vinaona kuwa, viongozi wa Umoja wa Ulaya kuamua kuahirisha kikomo cha siku ya kuidhinisha "Mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya" ni chaguo lao pekee lenye busara kwa ajili ya kuokoa mkataba huo.
Wachambuzi wameeleza pia kuwa, ingawa wameamua kuahirisha kikomo cha siku ya kuidhinisha mkataba huo, lakini uamuzi huo hauhusiki na utatuzi wa suala halisi la mustakbali wa "Mkataba wa katiba ya Umoja wa Ulaya", kama siku zijazo hali ya kukataliwa kwa mkataba huo itatokea tena, Umoja wa Ulaya namna itakavyokabiliana nayo, hili litakuwa tatizo lenye taabu litakalowakabili viongozi wa Umoja wa Ulaya.
Idhaa ya Kiswahili 2005-06-17
|