Mkuu mpya wa benki ya dunia Bw. Paul Wolfwitz tarehe 18 alimaliza ziara yake ya nchi nne barani Afrika nchini Afrika Kusini. Baada ya kufanya ukaguzi wa siku sita, anaona kuwa viongozi wapya wa Afrika wanapambana na ufisadi kwa kuwajibika zaidi na kuhimiza maendeleo ya taifa, uhusiano wa ushirikiano wa kiwenzi kati ya benki ya dunia na Afrika ni wa matumaini na fursa.
Baada ya kuwa mkuu wa benki ya dunia kwa wiki mbili, Bw. Paul Wolfwitz alizitembelea Nigeria, Burkina Faso, Rwanda na Afrika Kusini. Hatua hiyo ina lengo la kuthibitisha maoni yake kuwa, Afrika ni sehemu inayotiliwa mkazo na benki ya dunia kwa vitendo vyake halisi mwanzoni kabisa baada ya kushika madaraka hayo. Katika ziara yake hiyo, mkuu huyo alisikiliza maoni ya viongozi wa Afrika kuhusu namna ya kusaidia Afrika kupambana na umaskini na kuharakisha maendeleo na kutathmini mahitaji ya Afrika ya misaada kutoka nchi za nje.
Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini tarehe 18 alifanya mazungumzo na Paul Wolfwitz mjini Pretoria. Bw. Wolfwitz alisema baada ya kumaliza mazungumzo kati yake na Thabo Mbeki: "Katika siku sita hizo zilizopita, kadiri nilivyozitembelea nchi nyingi, ndipo nilivyoona kuwa kuanzisha ushurikiano na Afrika kuna fursa". Alisema kuwa viongozi wapya wa Afrika wanapambana na ufisadi kwa vitendo halisi na kushughulikia maendeleo ya taifa kwa kuwajibika. Hasa alitoa heshima kwa rais Mbeki aliyeanzisha harakati za kuadhibu ufisadi hivi karibuni nchini humo.
Mkutano wa wakuu wa nchi nane za magharibi utakaofanyika mwezi ujao nchini Uingereza utajadili hasa suala la kuongeza misaada kwa Afrika. Ingawa nchi zilizoendelea zikiongozwa na Uingereza zinafuatilia sana maendeleo ya Afrika, lakini zikitaja mpango halisi wa utoaji misaada, msimamo wao pia ni wazi kuwa nchi za Afrika zinapaswa kufikia lengo lililowekwa katika kupambana na ufisadi na kutekeleza utawala bora, ndipo zitakapoweza kupewa misaada mikubwa ya fedha.
Wachambuzi wanaona kuwa madhumuni mengine ya ziara ya Paul Wolfwitz barani Afrika ni kujua kuwa nchi za Afrika zinaweza kutumia misaada ya kimataifa kwa msimamo wa kuwajibika, na hilo ni suala linalofuatiliwa na nchi za magharibi zinazotoa misaada hiyo. Kutokana na matokeo ya ziara ya Paul Wolfwitz, tathmini iliyopata Afrika inaridhisha. Vyombo vya habari vinaona kuwa jambo hilo linasaidia mpango wa kuipatia misaada Afrika uungwe mkono kwenye mkutano wa wakuu wa nchi nane.
Kabla ya Paul Wofwitz kufunga safari tarehe 12 na kwenda nchini Nigeria kwa ziara, mkutano wa mawaziri wa fedha wa kikundi cha nchi nane za magharibi ulitangaza kufuta madeni yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 40 ya nchi 18 maskini, zikiwemo nchi 14 barani Afrika. Nchi za Afrika zimefurahia uamuzi huo, lakini pia zilitaka nchi zilizoendelea ziondoe vizuizi vya biashara. Bw. Wolfwitz aliunga mkono msimamo huo wa nchi za Afrika, akisema: "kama Rwanda nchi inayoendelea, inataka kuuza bidhaa nyingi zaidi katika soko la kimataifa, jambo hilo linazitaka nchi zilizoendelea zipunguze ruzuku kwa mazao ya kilimo na kufungua soko". Bw. Wolfwitz pia alieleza kuongeza nafasi za nchi za Afrika katika uamuzi wa mambo ya benki ya dunia.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-20
|