Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-20 16:40:49    
Mwandishi kijana Wang Zheng

cri

Katika miaka ya karibuni, nchini China wametokea waandishi wengi vijana, na wengi wao ni watunzi wa riwaya za Gongfu na za maisha ya ujana.

Katika nyanja ya utamaduni, mzee Wang Shirang mwenye umri wa miaka 90 anajulikana sana kutokana na utafiti wake wa mila na desturi za Wachina na samani za zama za kale, mwandishi kijana mwenye umri wa miaka 15 Wang Zheng ni mjukuu wake. Lakini umaarufu wa mwandishi huyo hautokani na babu yake bali kwa riwaya yake ya Gongfu "Mashujaa Wawili".

Wang Zheng ni mwanafunzi wa shule moja ya sekondari mjini Beijing. Kutokana na kuathiriwa na familia yake toka alipokuwa mtoto, alisoma riwaya nyingi maarufu za Kichina, na tabia hiyo ya kusoma inaendelea mpaka sasa. Wang Zheng alisema, "Kila siku natumia muda wa saa nne hadi saa tano kusoma, tabia hiyo nimeipata kutoka kwa baba yangu. Mama yangu huwa hajali kama ninafanya nini, ilimradi tu nifurahie ninachofanya."

Wang Zheng anapenda kusoma riwaya ndefu ya zamani "Ndoto kwenye Jumba Jekundu" na riwaya nyingine ambazo zote zinaeleza vituko vya mapenzi. Baada ya kujiunga na sekondari Wang Zheng alianza kusoma vitabu vingi vya riwaya za Gongfu na hamu ya kutunga riwaya ya Gongfu ilichipuka. Mwishoni mwa mwaka 2004 kwa juhudi za mwaka mmoja riwaya yake ya "Mashujaa Wawili" ilichapishwa. Kutokana na uzuri wa lugha na jinsi ilivyoelezea vituko, riwaya hiyo iliwavutia sana wasomaji.

"Mashujaa Wawili" ni riwaya iliyobuniwa na kutokea katika karne ya 13 nchini China. Riwaya hiyo ilisimulia jinsi mashujaa hao walivyopambana na wadhalimu na kuwatetea wanyonge, huku imechanganya mambo mengi ya mapenzi. Riwaya hiyo iliandikwa kwa lugha ya Kichina cha kale, ambayo ni kama riwaya iliyoandikwa na waandishi wa enzi za kale, ni vigumu kuamini kuwa riwaya hiyo kweli iliandikwa na kijana wa sasa mwenye umri wa miaka 15 tu. Lakini yeye mwenyewe alisema kwa unyenyekevu, "Labda nimejitokeza kidogo katika maandishi kwa kulingana na vijana wa rika yangu, na nilichoandika katika riwaya za Gongfu pia sio ya kawaida kwa sababu nimeingiza vituko vingi vya kimapenzi. Kwa kweli mimi sina maisha ya mapenzi, ufahamu wa mapenzi niyoandika unatokana kusoma vitabu vingi pamoja na fikra zangu mwenyewe."

Wang Zheng alisema, katika riwaya yake kitu anachotaka kueleza ni mapenzi yaliyowaka kwa kukutana tu na uhuru wake. Naona mapenzi yaliyowaka kwa kukutana tu mara ya kwanza ni mapenzi ya kweli, na uhuru wake ni jambo lolote wachumba wanalotaka kulifanya kwa kujiamulia wao wenyewe. Wang Zheng alisema riwaya yake ni ya riwaya kwa ajili ya watu wazima, anatumai wasomaji wanaposoma riwaya yake hawatafikiri kuwa ni riwaya iliyoandikwa na mtoto, bali watasoma riwaya yenyewe na kuipima kama kawaida bila kujali kama mwandishi mwenyewe ni mkubwa au mtoto.

Kutokana na kuandika riwaya, alipoteza wakati mwingi wa masomo shuleni, na baadhi ya wakati aliandika kwa usiku mzima, siku ya pili alishindwa kwenda shuleni. Kuhusu jambo hilo mwalimu wake alimsamehe sana, na Wang Zheng pia haoni masikitiko moyoni mwake. Alisema, "Kwa mtu wa kawaida, mtaka yote hukosa yote, ni vigumu kupata mambo yote kwa pamoja, labda inawezekana kwa wengine lakini mimi siwezi. Naandika riwaya sio kwa ajili ya kujiburudisha au kupitisha muda, leo naandika na kesho naiacha, bali nadhamiria kufanya kazi hiyo maishani mwangu, kwa hiyo lazima nitumie jasho langu na moyo wangu wote kufanya kazi hiyo, na mambo mengine nitayashughulikia ninapoweza tu."

Wang Zheng alisema, anatumai kuwa mwandishi wa kulipwa na atajitahidi kushiriki kwenye masomo ya shuleni.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-20