Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-20 21:54:22    
Dar es Salaam-Wananchi wa Tanzania wanaojitokeza kupima virusi vya ukimwi kuwa wachache

cri

Mkurugenzi wa elimu, habari na mawasiliano wa mpango wa taifa wa kudhibiti ukimwi nchini Tanzania, Dk. Benedict Fimbo alisema kuwa, asilimia 15 tu ya watanzania ndio wamejitokeza kupima virusi vya ukimwi katika vituo mbalimbali vya ushauri nasaha nchini.

Dk. Fimbo alisema asilimia hiyo ni ndogo, hivyo alishauri jitihada zifanyike kuhakikisha Watanzania wote wanajitokeza na kupima afya zao. Alisema kuwa serikali inaunga mkono juhudi hizo za utoaji huduma ya kupima kwa kuwa imekuwa ikitoa msaada mkubwa.