Tarehe 18 mwezi Juni makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Bw. Millgani na mwenyekiti wa muungano wa kidemokrasia wa taifa Bw. Ali Osman Taha walisaini makubaliano ya Cairo ya maafikiano ya kitaifa na amani ya pande zote. Hii ina maana kwamba, vita vya kisiasa vya miaka 15 kati ya serikali ya Sudan na Muungano wa kidemokrasia wa taifa vimemaliza. Sudan imepiga hatua kubwa katika mchakato wa kutimiza maafikiano ya kitaifa.
Rais Hosni Mubarak wa Misri, Rais Omar Bashir wa Sudan, kiongozi wa chama cha ukombozi wa umma cha Sudan Bw. John Garang walihudhuria mkutano huo. Rais Bashir alisema kuwa, serikali itakayoundwa na pande mbalimbali itaanzishwa tarehe 9 mwezi Julai, wakati huo mchakato wa kisiasa wa Sudan utaingia kwenye kipindi kipya. Bw. Millgani alisisitiza kuwa, hivi sasa Sudan inakabiliwa na fursa nzuri ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pande mbalimbali zinapaswa kuacha shughuli za kimabavu, kubeba majukumu ya amani na kufanya jitahada kwa pamoja ili kuijenga Sudan yenye muungano na ustawi.
Muungano wa kidemokrasia wa taifa ni chama kikubwa cha upinzani kaskazini mwa Sudan, ambacho kina vyama vya upinzani na jumuia mbalimbali za kisiasa 16. Miaka mingi iliyopita, chini ya msaada wa nguvu za nje, muugano wa kidemokrasia wa taifa ulikuwa unapambana na serikali ili kujipatia uhuru. Kutokana na mabadiliko ya hali ya Sudan na uhimizaji wa nchi mbalimbali zikiwemo Misri na Libya, mwezi Agosti mwaka 2004, muungano wa kidemokrasia wa taifa ulianzisha mchakato wa amani na serikali ya Sudan. Chini ya jitihada kubwa za pande mbili, mwezi Januari mwaka huu, ziliafikiana katika mada 13 za katiba, sheria na uchumi zinazohusika na mgawanyo wa madaraka ya nchi. Tarehe 12 mwezi huu, kutokana na mwaliko wa Misri, pande mbili zilifanya mazungumzo yanayofuata zaidi hali halisi huko Cairo. Duru la mwisho lilimalizika tarehe 18, masuala mengi yaliyobaki yametatuliwa, hivyo pande mbili zilisaini makubaliano ya Cairo.
Baada ya kusaini makubaliano hao, viongozi wa vyama vya upinzani ambao wanaishi nchi za nje wanatazamiwa kurudi Sudan na kufanya juhudi pamoja na serikali ili kusukuma mchakato wa maafikiano ya kitaifa. Rais Bashir alisihi watu wa Sudan wanaoishi nchi za nje watarudi Sudan kushiriki kwenye ujenzi wa nchi katika sekta za siasa, uchumi na jamii ili kufanya juhudi na kutoa mchango kwa aliji ya muungano, utulivu na ustawi wa Sudan. Rais Mubarak wa Misri ambaye alifanya juhudi kubwa katika kusukuma mbele mchakato wa amani ya Sudan alisema kuwa, kutokana na uzoefu wao, pande mbalimbali zilizosaini makubaliano zilifikia makubaliano kwa kauli moja, huu ni uhakikisho mkubwa kwa utekelezaji halisi wa makubaliano. Alizitaka pande mbalimbali zifanye jitihada kubwa kwa ajili ya muungano wa taifa na maisha bora ya wananchi.
Wakati huo huo, watu wangetambua kwamba, bado kuna vyama kadhaa vya upinzani ambavyo havijasaini makubaliano ya amani. Gazeti la Misri la Pyramid tarehe 19 mwezi Juni liliripoti kuwa, bado kuna masula mawili hayajatatuliwa, moja ni jinsi shirikisho la kidemokrasia la taifa linavyoingia katika idara za serikali; nyingine ni namna ya kushughulikia suala kuhusu jumuia za kijeshi chini ya shirikisho hilo. Kutokana na nyongeza za makubaliano, kama masuala hayo mawili hayatatuliwa, makubaliano hayo hayatafanya kazi.
Rais Bashir wa Sudan alisema kuwa, mwaka huu ni mwaka wa amani, utulivu na muungano wa taifa kwa Sudan. Ili kutimiza lengo hilo, Sudan imeanzisha kamati tatu za kushughulikia utekelezaji wa makubaliano.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-21
|