Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-21 16:21:29    
Ziara ya kuboresha sura yake ya Bw Wolfwitz barani Afrika

cri

Mkurugenzi mpya wa Benki ya dunia Bwana Paul Wolfwitz hivi karibuni amemaliza ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu ashike madaraka yake. Ziara yake hiyo barani Afrika pia ni ziara ya kuboresha sura yake.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa mkurugenzi wa benki kuu ya dunia, Bwana Wolfwitz akiwa ofisa muhimu wa idara ya jeshi la Marekani, aliwahi kushika wadhifa wa naibu waziri wa ulinzi wa Marekani kwa awamu mbili, na alichukuliwa kuwa ni mtu muhimu wa "kundi la tai" la serikali ya Marekani, pia alikuwa mmoja kati ya wakuu waliotoa maamuzi kuhusu sera ya kijeshi ya Marekani, hata wengine walimwita msanifu mkuu na mwungaji mkono mwenye nguvu kwa Marekani kuanzisha vita dhidi ya Iraq. Ndivyo hivyo, tarehe 16 Machi mwaka huu wakati rais Bush wa Marekani alipomteua Bw Wolfwitz kuwa mkurugenzi mpya wa Benki ya dunia, mara moja uteuzi huo ulilaumiwa na nchi kadhaa na jumuiya kadhaa za kimataifa. Kwa upande mmoja, watu walitia mashaka juu ya uwezo wa Wolfwitz, waliona kuwa kazi alizowahi kufanya nyingi zilihusika na mambo ya kidiplomasia na mambo ya ulinzi wa taifa, na hana uzoefu wa kuzisaidia nchi zinazoendelea, kwa hiyo ni vigumu kwake kuisaidia Benki ya Dunia kutimiza nia yake ya kuzisaidia nchi ambazo uchumi wao bado uko nyuma kutimiza maendeleo ya uchumi. Lakini Rais Bush alimteua Wolfwitz kuwa mkurugenzi wa Benki ya dunia ambayo idara muhimu ya fedha ni kwa ajili ya kumsifu kutokana na "uhodari wake" katika vita dhidi ya Iraq; kwa upande mwingine, watu walikuwa na wasiwasi kuwa Wolfwitz aliyekuwa mtu mwenye nguvu katika idara ya kijeshi ambaye siku zote anatetea kuwa Marekani inapaswa kutumia hadhi yake ya nchi kubwa kwa kusukuma mbele mageuzi ya nchi nyingine, kama akishika madaraka ya benki ya dunia, huenda ataongeza masharti ya kisiasa atakapotoa mikopo kwa nchi zinazoendelea. Hata baada ya kushika madaraka ya benki ya dunia kwa Wolfwitz, pia kulikuwa na watu walioona kuwa, kazi ya benki ya dunia ya siku zijazo itakabiliwa na hatari ya kwenda mrama.

Ili kuondoa wasiwasi wa watu na kuboresha sura yake mwenyewe, Bw Wolfwitz alifanya kazi kubwa. Kabla ya kuchaguliwa kuwa mkurugenzi wa benki ya dunia, aliwaahidi mara kwa mara waandishi wa habari na mameneja wa benki ya dunia kwamba, kama atashika madaraka ya benki ya dunia, hakika hataweza kuilazimisha benki ya dunia kupokea ajenda ya Marekani, na hata aliahidi kuwa atafanya juhudi za dhati katika shughuli za maendeleo na kuondoa umaskini duniani. Mwanzoni mwa mwezi huu, Bw Wolfowitz alipoanza kushika madaraka ya benki kuu, mara alikiri kwa unyenyekevu kuwa yeye bado anatakiwa kujifunza mambo mengi. Kwa hiari aliongea na watumishi wa benki wakati alipokutana nao katika benki, alitangaza anuani yake kwenye mtandao wa internet, na kuwakaribisha watumishi kutoa maoni yao ili kunyamazisha ukosoaji kwake; tena alitangaza kuwa siku zijazo atafanya juhudi zote barani Afrika ili kutatua suala la umaskini wa Afrika, na kuziwezesha nchi maskini zipate manufaa mengi. Alitoa matumaini yake kuwa katika kipindi chake cha madaraka, benki ya dunia itaisaidia Afrika kuelekea kuwa "Bara lenye matumaini" badala ya "Bara la kukata tamaa".

Ndiyo maana, katika siku ya 7 baada ya kushika madaraka ya benki ya dunia, Bw Wolfwitz alitangaza kuwa atafanya ziara nchini Nigeria, Burkina fasso, Rwanda na Afrika ya kusini ili kuonesha nia yake kuwa "Afrika ni sehemu muhimu inayofutiliwa na benki ya dunia." Katika ziara yake, Bw Wolfwitz alisikiliza maoni ya viongozi wa Afrika kuhusu namna ya kuisiadia Afrika kuondokana na umaskini na kuharakisha maendeleo, pia alitathmini mahitaji ya Afrika ya misaada kutoka nje.

Yote hayo yameonesha kuwa, Bw Wolfowitz alitumia fursa ya ziara yake ya nchi 4 za Afrika kufanya chini juu kwa kuondoa sura yake ya zamani ili kujitoa kutoka kwenye athari isiyomsaidia na kuonesha sura mpya ya mkurugenzi wa benki ya dunia.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-21