Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-21 16:31:01    
Watu wa Guinea Bissau wanatumai uchaguzi mkuu utawaletea maisha ya utulivu

cri

Uchaguzi mkuu wa Guinea Bissau ulifanyika tarehe 19 kama ilivyopangwa. Watu wa Guinea Bissau wanatumai kuwa uchaguzi huo utawaletea maisha ya utulivu.

Watu laki 5.38 walipiga kura, watamchagua rais mpya kutoka wagombea 13, matokeo ya uchaguzi huo yatatangazwa baada ya siku kumi.

Guinea Bissau ni nchi ndogo kwenye ukingo wa Bahari ya Atlantiki, eneo lake ni kilomita za mraba elfu 36 na ina watu milioni 1.3. mazao ya nchi hiyo ni korosho, samaki na mchele. Na pia kuna madini mengi na mafuta ambayo bado hayajachimbuwa. Tokea mwaka 1974 Guinea Bissau ilipopata uhuru, uasi ulitokea mara nyingi. Katika miaka ya 90, wimbi la mfumo wa vyama vingi lilivuma barani Afrika, mapambano kati ya vyama yalikuwa makali kila baada ya siku, na wanajeshi waliingilia mambo ya serikali, uchumi ulizorota vibaya, na jamii ilijaa machafuko. Hivi sasa mapato ya taifa yameshuka hadi dola za Kimarekani 130 kwa wastani wa kila mtu kwa mwaka kutoka 250, na ongezeko la uchumi limeshuka hadi sufuri kutoka 5%, na wastani wa umri wa kuishi kwa ni miaka 45 tu. Watu wasiojua kusoma na kuandika wanachukua 70%, maendeleo ya binadamu yanachukua nafasi ya tano kutoka nyuma kati ya nchi zote 177 duniani.

Kabla ya uchaguzi mkuu waandishi wa habari walikwenda huko na kujionea hali mbaya iliyosababishshwa na machafuko. Nchini humo hakuna hata barabara moja inayoridhisha, maduka karibu yote ni vibanda, bidhaa ni chache sana ambazo hata za maisha ya kila siku ni za ng'ambo, umeme ni nadra sana kupatikana siku nzima, hata waandishi wa habari hawawezi kutuma habari zao kutokana na ukosefu wa umeme. Baada ya giza kuingia, mji mzima unagubikwa na giza totoro, wapita njia ni wachache sana. Watu wasio na ajira wanachukua 60%, na mshahara wa ofisa wa serikali kwa wastani kila mwezi ni faranga za Afrika 150 ambazo ni kiasi cha dola za Kimarekani 25. Hali ilivyo ya Guinea Bissau imethibitisha kuwa "maendeleo hayapatikani bila ya hali ya utulivu".

Hali ya machafuko katika miaka 30 iliyopita nchini Guinea Bissau imeonesha kuwa mfumo wa kidemokrasia wa nchi za Magharibi uliopandwa barani Afrika haukuchipuka kila mahali, mapambano ya kugombea maslahi na madaraka kati ya makabila na vyama hayaishi, na kusababisha hali mbaya ya maisha ya wananchi, lakini nchi kubwa za Magharibi zinapata faida kutoka mapambano hayo.

Mtaalamu wa mambo ya Guinea Bissau wa Afrika Kusini alisema, kwa kisingizio cha kutoa msaada viongozi wanawalea vibaraka wao ili kudhibiti shina la uchumi na maliasili za nchi hiozo, hivi sasa Marekani imeweka nchi za Afrika Magharibi ikiwemo Guinea Bissau kuwa ni ghala la mafuta.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-21