Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-22 16:22:11    
Mkutano wa viongozi wa Palestina na Israel haukufanikiwa sana

cri

Tarehe 21 mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw. Mahmood Abbas na waziri mkuu wa Israel Bw. Sharon walikutana kwa mara ya pili tokea mwezi Februali kwa lengo la kujadiliana utekelezaji wa mpango wa upande mmoja, lakini mkutano huo haukufanikiwa sana.

Mkutano ulifanyika kwa muda wa saa mbili. Baada ya mkutano huo viongozi hao wawili hawakukutana na waandishi wa habari kama kawaida yao, Bw. Abbas aliondoka haraka kwa gari lake. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana baadaye, mkutano huo haukuwa na maana sana.

Kwenye mkutano Bw. Sharon alitoa ahadi mfululizo: Israel itakubali kukabidhi haki ya kudhibiti miji ya Bethlehem na Qalqilyah; itakubali Palestina ifungue uwanja wa ndege wa Gaza na forodha yake; itakubali watu kadhaa wenye silaha wa Palestina waliofukuzwa hadi Gaza warudi kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Jordan na kufikiria kuwaachia huru wafungwa wengi zaidi wa Palestina. Lakini yote hayo hayatatekelezwa iwapo Palestina itashindwa kuhakikisha usalama wa Waisrael wanapoondoka kutoka Gaza bila kushambuliwa na watu wenye silaha wa Palestina.

Kwenye mkutano Bw. Sharon aliishutumu wazi Palestina kisema kuwa, tokea mwezi Februari mapatano ya kusimamisha vita yalipopatikana, Palestina inaonekana kuwa "haijafanya kazi yoyote" dhidi ya mashambulizi ya kisilaha, na kumkosoa Bw. Abbas kuwa ni "mnyonge" mbele ya vikundi vyenye siasa kali. Lakini Abbas pia aliilalamikia Israel. Baada ya Abbas kurudi mjini Ramallah hakuonana na waandishi wa habari kama mpango ulivyopangwa bali alimwagiza waziri mkuu wake Ahmed Qurie awaeleze waandishi wa habari. Kwenye mkutano na waandishi wa habari Bw. Ahmed Qurie alisema, mkutano ulifanyika kwa taabu, viongozi wa Palestina na Israel hawakutatua masuala yoyote muhimu. Na Israel haikuonesha chochote kuhusu masuala yaliyotolewa na Palestina.

Kuhusu matokeo ya mkutano huo watu hawaoni ajabu. Kabla ya mkutano, pande mbili zilikuwa na maoni tofauti kuhusu mada ya mkutano huo, kwamba Israel ilitaka Palestina iweke mpango kuhakikisha usalama wa Wayahudi wanapoondoka Gaza na wasishambuliwe na vikundi vyenye silaha, na sehemu ya Gaza isiwe sehemu ya vikundi hivyo. Palestina inataka Israel iweke ratiba ya kuikabidhi haki ya kumiliki Gaza na kuhakikisha mawasiliano huru ya bidhaa na wasafiri. Isitoshe, Palestina inataka Israel iendelee kukabidhi miji ya magharibi ya Mto Jorden na kusimamisha vitendo vya kijeshi kuhujumu watu wenye silaha wa Palestina, isimamishe kujenga ukuta wa utenganisho na kuendelea kuwaachia huru wafungwa wa Palestina na kuondoa vituo vya ukaguzi mpakani. Mapema kabla ya mkutano huo, Bw. Sharon aliwahi kuwaambia waandishi wa habari akisema, "Mimi sitahudhuria mkutano na karoti, na Israel haina matumaini kama mkutano huo utakuwa na mafanikio yoyote. Mbele ya hali ya hivi sasa Israel haina haja kumpa Abbas karoti, tunatumai Bw. Abbas aeleze jinsi atakavyofanikiwa kuzuia mashambulizi ya silaha."

Lakini kwa upande mwingine, bado kuna muda wa miezi miwili kabla ya kutekeleza mpango wa upande mmoja. Sababu ya Bw. Sharon kutaka Abbas apambane na vikundi vyenye siasa kali inaonesha wasiwasi wake kama Wayahudi wataondoka Gaza salama. Kwa ajili ya usalama, Israel inataka ushirikiano na Palestina. Isitoshe, kitu kinachostahili kufuatiliwa ni kuwa Hamas yenye athari kubwa kisiasa itaivumilia Israel kutokana na kutaka kushiriki kwenye kamati ya kutuga katiba na kujiingiza katika mambo ya siasa.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-22