Mazungumzo ya kwanza kati ya Asia na Mashariki ya kati yalifanyika kuanzia tarehe 21 hadi 22 huko Singapore, ambapo wajumbe zaidi ya 200 kutoka nchi na sehemu 40 ikiwemo China walikusanyika kujadili masuala mawili makubwa ya maendeleo na ushirikiano kati ya sehemu hizo mbili zenye nguvu kubwa, na wamepata maoni ya pamoja kuhusu masuala mengi. Mazungumzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya sehemu hizo mbili hata kwa maendeleo ya dunia nzima.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni "Maslahi ya pamoja na changamoto za pamoja", madhumuni yake ni kuiimarisha mazungumzo na maelewano kati ya Asia na sehemu ya mashariki ya kati, na kuongeza ushirikiano wenye mafanikio kati ya sehemu hizo mbili kwenye sekta mbalimbali.
Mawasiliano kati ya Asia na sehemu ya Mashariki ya kati yalianza tangu enzi na dahari, hivi leo katika hali ambayo mabadiliko mengi yenye utatanishi yanatokea duniani, kutafuta amani, kuhimiza maendeleo na kutaka ushirikiano kumekuwa sauti kubwa na mawimbi makuu. Na maendeleo ya kasi ya ncha nyingi na utandawazi wa uchumi duniani pamoja na hali ambayo nchi mbalimbali duniani zinazidi kutegemeana siku hadi siku, hayo yote yameleta fursa ya kihistoria ambayo ni nadra kupatikana kwa ushirikiano kati ya Asia na Mashariki ya kati.
Nchi nyingi kabisa za Asia na Mashariki ya kati ni nchi zinazoendelea, ambazo zina matumaini ya pamoja kuhusu amani, usalama, utulivu na ustawi. Ndiyo maana nchi hizo zina maoni ya pamoja au yanayofanana kuhusu masuala mengi makubwa ya kimataifa na kikanda, na tena zina maslahi mengi ya pamoja.
Kwenye mkutano huo, kiongozi wa ujumbe wa China Bwana Ma Zhengang alifafanua mapendekezo ya serikali ya China kuhusu kuimamrisha uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano kati ya Asia na Mashariki ya kati. Alisema kuwa, China inatilia maanani na kuunga mkono mazungumzo kati ya Asia na Mashariki ya kati, inapenda kufanya juhudi kubwa na kushirikiana na nchi za Asia na Mashariki ya kati katika kusukuma mbele maendeleo mazuri ya mazungumzo kati ya Asia na Mashariki ya kati, na kuimarisha ushirikiano kati ya sehemu mbili kubwa za Asia na Mashariki ya kati. Alisema, Asia na Mashariki ya kati zinapaswa kufuata moyo na kanuni za kuwa na usawa na kunufaishana, kupiga hatua kwa utaratibu na kutafuta maendeleo kwa pamoja. Sehemu hizo mbili zingefuata hali halisi ya sehemu hizo na kuenzi vilivyo hali bora za sehemu hizo, kusaidiana na kuhimiza maingiliano na ushirikiano kati ya sehemu hizo katika sekta mbalimbali. China ina imani kuwa, bila kujali mabadiliko ya namna gani yanayotokea duniani, China na nchi za mashariki ya kati daima ni marafiki na wenzi wazuri. Hivyo China imetoa mapendekezo manne kuwa sehemu hizo mbili zingeheshimiana na kusaidiana kisiasa; kufanya ushirikiano wa kiuchumi kwa kufuata hali halisi ili kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja; kufundishana kiutamaduni; kuwa na usawa na uaminifu katika mambo ya usalama na kufanya mazungumzo na mashauriano. Mapendekezo hayo ya China yameonesha nia na matumaini ya wajumbe wa nchi zilizohudhuria mkutano huo.
Kuhusu mada za siasa na usalama, wajumbe wengi walisisitiza kuwa amani, maendeleo, utulivu na usalama ni mambo yanayohusiana na yasiyoweza kutenganishwa. Wajumbe hao wanaona kuwa lazima kuimarisha mazungumzo ya dhati na ushirikiano wenye ufanisi ili kupambana kwa pamoja dhidi ya matishio mbalimbali ya kijadi na yasiyo ya kijadi, na kulinda amani ya kikanda na dunia.
Hivi sasa Asia na Mashariki ya kati zote ziko katika kipindi muhimu cha kihistoria, kuimarisha mazungumzo hakika ni mwanzo mzuri wa kuongeza uaminifu na mawasiliano ili kupata maendeleo ya uchumi kwa pamoja.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-23
|