Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-23 12:23:22    
Watu wengi zaidi wa Japan wapinga waziri mkuu Koizumi kwenda hekalu kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita

cri

Hivi karibuni nchini Japan, raia wa kawaida na maofisa wa serikali wengi zaidi wanapinga waziri mkuu Junichiro Koizumi kwenda tena kwenye hekalu kutoa heshima kwa wahalifu wa kivita. Gazeti la Mainichi Shinbun la Japan tarehe 20 lilitoa matokeo ya uchunguzi wa maoni ya raia yakionesha kuwa, asilimia 50 ya wananchi wa Japan wanapinga kitendo hicho cha waziri mkuu.

Katika idara za siasa za Japan, baadhi ya watu wenye athari pia wamejitokeza kumtaka Bw Koizumi aache kwenda kwenye hekalu hilo kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita. Bwana Tsuyoshi Noda aliyekuwa waziri wa ujenzi na waziri wa mambo ya kujiendesha wa Japan ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa Shirika la Japan na China tarehe 22 alipohojiwa na mwandishi wa habari alisema kuwa, kwenye hekalu la Yasukuni inaabudiwa mizimu ya wahalifu wa kivita wa ngazi ya A, kutokana na hali hiyo tu, Bw Koizumi anapaswa kuzingatia mambo makuu na kuacha kwenda kwenye hekalu hilo. Bwana Noda alisema, kwa Koizumi kwenda kwenye hakalu hilo kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita au la ni kikwazo kikuu katika mambo ya kidiplomasia ya Asia.

Kabla ya hapo, watu wenye athari kubwa katika idara za siasa za Japan pia walimsihi Bw Koizumi aache kwenda kwenye hekalu. Tarehe 1 Juni, spika wa baraza la chini la bunge la Japan Yohei Kono na mawaziri wakuu wa zamani Toshiki Kaifu, Kiichi Miyazawa, Tomiichi Murayama, Ryutaro Hashimoto na Yoshiro Mori pia walitoa maoni yao kuhusu uhusiano kati ya Japan na China na kati ya Japan na Korea ya kusini. Waliona kwa kauli moja kuwa, Junichiro Koizumi kwenda kwenye hekalu kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita ni sababu kubwa ya kuleta hali mbaya ya uhusiano kati ya Japan na nchi jirani zake, walimtaka Bw Koizumi azingatie kwa makini na kuchukua tahadhari tena na tena kuhusu suala hilo. Tarehe 7 Juni, Bwana Yohei Kono alimwambia Bw Koizumi kuhusu maoni ya mawaziri wakuu hao wa zamani. Vyombo vya habari vya Japan vilitoa maelezo kuwa, hali hiyo ni nadra kutokea katika historia ya Japan, ambayo imeonesha kuwa viongozi wazee wa chama cha uhuru na demokrasia cha Japan wametambua hali mbaya inayoletwa na suala hilo.

Na waziri mkuu wa zamani Bwana Yasuhiro Nakasone tarehe 1 na 2 Juni alitoa matamko mfululizo akimtaka Bw Koizumi awe na ujasiri wa kuacha kwenda hekalu kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita ili kuiepusha Japan kupoteza fursa ya kuwa mjumbe wa kudumu kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Hivi karibuni Bwana Nakasone amesema tena kuwa, kitendo cha Koizumi kitaifanya nchi ipoteze mwelekeo wa kusonga mbele. Katibu mkuu wa zamani wa chama cha uhuru na demokrasia cha Japan Hirokazi Kato tarehe 2 Juni pia alisema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika huko Tokyo kuwa, kama Japan ikitaka kuwa mjumbe wa kudumu kwenye baraza la usalama, Bw Koizumi ni lazima aache ati itikio lake mwenyewe, na kudumisha uhusiano wa kirafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Japan na China na Japan na Korea ya kusini.

Waziri mkuu wa zamani wa Japan Kiichi Miyazawa tarehe 19 Juni alipohojiwa na mwandishi wa habari wa Kituo cha televisheni cha Asahi cha Japan alisema kuwa, kitendo cha Bw Koizumi kimekwamisha mawasiliano kati ya viongozi wa Japan na China, ni lazima Bw Koizumi azingatie kwa makini kutokana na kuboresha uhusiano kati ya Japan na China.

Watu wengi wa nchini Japan wana wasiwasi kuwa, Bw Koizumi akiendelea kwenda kwenye hekalu kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita, kitendo chake kitafanya uhusiano kati ya Japan na China na Korea ya kusini uliodhuriwa uzidi kuwa mbaya, tena kutaiathiri Japan isiweze kuwa mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-23