Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-23 15:59:46    
Bei ya mafuta katika soko la kimataifa yaendelea kupanda

cri
Kuanzia mwezi Juni, bei ya mafuta imeendelea kupanda katika soko la kimataifa na kuweka rekodi ya juu kabisa katika historia. Bei ya mafuta ya wakati ujao katika kituo cha biashara cha New York imekaribia dola za kimarekani 60 ambayo imezidi ile ya mwaka jana kwa zaidi ya asilimia 50, hali hiyo inafuatiliwa sana na pande mbalimbali. Ingawa bei hiyo ilipungua kidogo tarehe 22, lakini watu wanaoshughulikia biashara waliainisha kuwa bei hiyo itaendelea kuwa ya juu katika nusu ya pili ya mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa tarehe 22 na wizara ya nishati ya Marekani kuhusu akiba ya mafuta ni sababu moja ya kupungua kwa bei ya mafuta siku hiyo, kwani hali ya akiba ya mafuta nchini Marekani ni nzuri zaidi kuliko vile ilivyokadiriwa.

Zaidi ya hayo, nchi kubwa ya tatu duniani inayouza mafuta kwa wingi katika nchi za nje Norway ilifaulu kuzuia mgomo wa wafanyakazi wa mafuta wa nchi hiyo, na pande mbili za wafanyakazi na waajiri zilifikia makubaliano kuhusu mishahara ya wafanyakazi, jambo ambalo lilipunguza kidogo bei ya mafuta kwa kiasi fulani.

Lakini watu wengi wa sekta hiyo waliainisha kuwa, ingawa bei ya mafuta ilipungua kidogo, lakini vyanzo vingi vinadhibiti bei ya mafuta na kuifanya iwe kubwa.

Kwanza, jumuiya ya kimataifa inakosa imani kwa kiasi cha utoaji wa mafuta. Uhusiano kati ya utoaji na mahitaji ni chanzo cha msingi cha kudhibiti bei ya mafuta. Kadiri uchumi unavyoendelezwa duniani, ndipo mahitaji ya mafuta duniani yanavyongezeka siku hadi siku. Wakati huo huo, jumuiya ya kimataifa ina mashaka kuhusu uwezo wa uzalishaji mafuta wa OPEC. Ingawa OPEC ilifanya uamuzi tarehe 15 mwezi huu kuwa kuanzia tarehe mosi mwezi Julai, itaongeza kiasi cha uzalishaji mafuta wa kila siku hadi kufikia mapipa milioni 28 kutoka mapipa milioni 27.5 ya hivi sasa, lakini uamuzi huo haukusaidia katika kupunguza bei ya mafuta, kwani nchi nyingi wanachama za OPEC hazina uwezo wa kuongeza zaidi kiasi cha uzalishaji mafuta.

Pili, mambo yasiyotulia yanaathiri bei ya mafuta. Ingawa athari ya mgomo wa kazi nchini Norway imeondolewa, lakini habari mbaya imetokea katika nchi kubwa kabisa inayouza mafuta barani Afrika, Nigeria, dhehebu moja kubwa ya kabila nchini humo lilitangaza kufanya mgomo wa kazi wa siku tatu katika wiki kadhaa zijazo.

Tatu, ni magendo ya kibiashara. Utoaji na mahitaji kwenye soko la mafuta duniani vinawiana, lakini kuna fedha nyingi za kufanya magendo katika soko la kimataifa, fedha hizo zinaweza kuleta machafuko kwenye soko. Wataalam wanakisia kuwa katika bei ya mafuta ya hivi sasa, dola za kimarekani zisizopungua 10 kwa kila pipa zinatumika katika kufanya magendo.

Vyombo vya habari vimeainisha kuwa, suala la kudhibiti bei ya mafuta haliwezi kutatuliwa na jumuiya fulani au nchi fulani bali linapaswa kutatuliwa na jumuiya ya kimataifa kwa pamoja.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-23