Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-23 20:22:31    
Mji wa Lhasa

cri

Mji wa Lhasa ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Tibet uko katika tambarare ya sehemu ya katikati ya mto Lhasa ambao ni tawi la Mto Yarlung Zangbo. Uko katika longitudo ya mashariki digrii 91'07" na latitudo ya kaskazini 29'39", urefu wake kutoka usawa wa bahari ni mita 3658. Katika mji huo hali ya hewa ni nzuri kwa mwaka mzima, hakuna bardi kali katika majira ya baridi wala joto kali katika majira ya joto. Na hali ya hewa huko ni ya nusu ukame ya pepo za misimu ya uwanda wa juu. Mvua hunyesha katika miezi ya Julai, Agosti na Septemba. Mjini humo kuna hewa safi na mwangaza wa jua wa kutosha, hivyo Lhasa inasifiwa kuwa mji wa mwangaza wa jua na ni moja wa miji iliyoko kwenye urefu mkubwa zaidi kutoka usawa wa bahari na hewa safi duniani.

Mji wa Lhasa ulianza kujengwa katika karne ya 7, kabla ya hapo uliitwa Womatang, ambao ulikuwa ni malisho ya mifugo ya kabila la Supi. Katika karne ya 7, baada ya Songtsan Gambo kuunganisha Tibet na kuanzisha dola la kifalme la Tubo, alihamisha mji mkuu kutoka mji wa Shannan hadi Lhasa, na kujenga hekalu la Jokhang, hekalu la Ramoche, na kasri la Potala. Kutokana na ustawi wa dini ya Kibudha, watu wa Tibet wanauchukulia mji huo kuwa ni mji mtakatifu.

Baada ya dola la kifalme la Tubo kusambaratika katika karne ya 9, kutokana na ustawi wa Dini ya Kibudha katika karne ya 11, mji wa Lhasa ulikuwa sehemu ambayo malamawengi maarufu walieneza wazo la dini ya kibudha. Katika karne ya 13, serikali kuu ya Enzi ya Yuan iliingiza sehemu ya Tibet katika ramani yake. Katika katikati ya enzi ya 17, Dalai Lama wa tano Lobsang Gyaco alithibitishwa na mfalme wa Enzi ya Qin, na kuanzisha utawala wa utumwa wa kimwinyi. Mji wa Lhasa ulikuwa mji mkuu wa utawalahuo, na ulipata maendeleo mapya. Mahekalu mengi maarufu yalifanyiwa ukarabati upya na kupanuliwa katika kipindi hicho. Kasri la Potala ilijengwa upya, baadaye lilikarabatiwa na kupanuliwa. Wakati Dalai Lama wa Saba aliposhika madaraka, Bustani ya Norbulinka ilijengwa magharibi ya kasri la Potala, baadaye ilipanuliwa na kuwa bustani mkubwa yenye eneo la mita za mraba laki 3.6.

Kuna na masalio mengi ya kihistoria na vivutio vya kitalii mjini Lhasa. Mandhari ya kijiografia ya huko ni nzuri, kuna vilele vya milima vinavyofunikwa na theluji na barafu nyeupe, mbuga, maziwa makubwa, ukungu kutokana na joto la ardhini, ardhi oevu na misitu. Na Mjini humo kuna mahekalu zaidi ya 200, mabaki ya kale yenye historia zaidi ya miaka elfu 1. Majengo ya kale yenye eneo la kilomita za mraba 1.3 yakiwemo kasri la Potala na hekalu la Jokhang yamewekwa kwenye orodha ya urithi wa utamaduni duniani na Shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa, na yanaheshimiwa na kuhifadhiwa na binadamu wote.  

picha husika >>

1  2