Wataalamu wanne wanaofanya uchunguzi huru kuhusu suala la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, tarehe 23 walilishitaki jeshi la Marekani kuwa na vitendo vingi vya kuwadhalilisha wafungwa katika kituo cha Guantanamo, na kuilaumu Marekani kwa kuwazuia wataalamu hao wasiende kwenye kituo cha Guantanamo kufanya uchunguzi. Ingawa idara husika ya Marekani ilikanusha shutuma hizo, lakini ushahidi mwingi umeonesha kuwa, kukataa huko kwa Marekani kumedhihirisha zaidi ukweli wa jeshi la Marekani kuwadhalilisha wafungwa.
Habari zinasema kuwa, wataalam hao wanne kutoka Algeria, Argentina, Austria na New Zealand mwaka 2002 walikabidhiwa madaraka na Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi huru wa miaka mitatu kuhusu jeshi la Marekani kuwadhalilisha wafungwa. Tarehe 23, kwenye mkutano wa wakimbizi wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Geneva, wataalam hao wanne walitoa taarifa ikisema kuwa, ushahidi mwingi umethibitisha kuwa, kwenye kituo cha jeshi la Marekani cha Guantanamo, zilitokea shughuli nyingi katili na zisizokuwa za kiutu za kuwadhalilisha wafungwa, Marekani kamwe haizingatii afya na haki za wafungwa. Wataalamu hao walisema kuwa, kuanzia mwaka 2002, maombi yao mengi ya kutaka kwenda kwenye vituo vya jeshi la Marekani vya Guantanamo, Iraq na Afghanistan kufanya uchunguzi yalikataliwa, msimamo huo wa Marekani wa kukataa kushirikiana umeonesha kidhahiri kuwa, serikali ya Marekani inajaribu kuficha ukweli wa mambo.
Kutokana na lawama hizo, msemaji wa Marekani huko Geneva Bi.Brooks Robinson alisema kuwa, kutojibu kwa wakati ombi la wataalam hao la kwenda kwenye kituo cha Guantanamo kufanya uchunguzi kumeonesha kuwa, Marekani imeshafanya uchunguzi kamili kuhusu mambo hayo. Sera ya Marekani inapiga marufuku kuwadhalilisha wafungwa, serikali ya Marekani imekuwa ikizingatia ombi lao la kwenda kituo cha Guantanamo kufanya uchunguzi.
Kuanzia mwezi Januari mwaka 2002, jeshi la Marekani liliwapeleka watuhumiwa wa ugaidi wa serikali ya zamani ya Taliban na kundi la Al-Qaeda waliokamatwa nchini Afghanistan na Pakistan kwenye gereza la Guantanamo. Hivi sasa ndani ya gereza hilo kuna wafungwa 520 kutoka nchi zaidi ya 40, na wengi wao wameshafungwa huko miaka 3 na zaidi, lakini bado hawajahukumiwa kwa hatia yoyote. Katika kipindi hicho, mashirika mbalimbali ya kimataifa na vyombo vya habari mara kwa mara vimedokeza vitendo kuhusu kunyanyaswa kwa wafungwa vya gereza hilo. Na tukio lililodokezwa na jarida la News Week la Marekani mwezi Mei mwaka huu kuhusu askari wa Marekani kudhalilisha Kurani, pamoja na toleo maalum lililotolewa tarehe 12 mwezi huu na jarida la Time la Marekani kuhusu jinsi askari wa Marekani walivyowadhalilisha wafungwa yamesababisha lawama nyingi zaidi za jumuiya ya kimataifa dhidi ya Marekani, na kituo cha Guantanamo kimekuwa shabaha iliyochukizwa na waislamu. Watu wengi mashuhuri wa Marekani wakiwemo marais wa zamani James Carter na Bill Clinton kwa nyakati tofauti walitaka kituo hicho kifungwe.
Lakini rais George Bush, waziri wa ulinzi Donald Rumsfeld na maofisa wengine wa ngazi ya juu wa Marekani siku zote wanakanusha kithabiti habari hizo.
Nchi nyingi duniani na mashirika ya kimataifa yamelaani vikali msimamo huo wa Marekani. Vyombo vya habari vimeainisha kuwa, serikali ya Marekani ilikataa kukiri vitendo vya kuwadhalilisha wafungwa, au kusisitiza kuwa, vitendo vya kuwadhalilisha wafungwa ni vya watu wachache tu. Jambo hilo limeonesha kuwa, serikali ya Bush inapuuza sheria na katiba ya kimataifa, kamwe haikuzingatia kwa makini matukio ya kuwadhalilisha wafungwa. Na imeonesha kwa mara nyingine tena kuwa, Marekani inachukua msimamo wa ubabe na vigezo tofauti kuhusu haki za binadamu.
|