Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-24 18:39:45    
Kikosi cha China cha ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

cri

 

Kundi la tatu la vikosi vya uhandisi na matibabu vya ulinzi wa amani vya China liliwasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mwezi Agosti, mwaka 2004. Wakati Kikosi cha uhandisi cha China kilipofika kwenye kituo cha kijeshi kilichoko katika kitongoji cha Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu ya Kusini, mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, kilikabiliwa na hali ya fujo baada ya vita, ambapo mvua kubwa, na hali mbaya ya mmomonyoko wa ardhi ziliharibu vibaya barabara inayounganisha mji wa Boukavu na Uwanja wa Ndege wa nchi hiyo. Hali iliyowasikitisha zaidi ni kuwa, Ujumbe maalum wa Umoja wa Mataifa hakutoa saruji wale mawe yaliyohitajika kwa ujenzi mpya wa barabara. Kutokana na hali hiyo, Kikosi cha Uhandisi cha China kiliwashawishi wenyeji wa huko kuwaruhusu kuchimba mawe kwenye uwanja mmoja. Baada ya kufanya juhudi za muda usiozidi mwezi mmoja, kikosi cha uhandisi cha China kilijenga upya barabara hiyo, ambapo kasi ya gari iliongezeka hadi kilomita 40 kwa saa kutoka kilomita 10 kwa saa. Baada ya hapo, walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa na wananchi wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo hukisifu kikosi cha uhandisi cha China kila wanapokutana nacho.

Kwa kuwa tume ya Umoja wa Mataifa hakuwapatia picha nzuri watu wa Jamhuri ya Kidemokasi ya Kongo, ili kuepuka migongano na wenyeji wa huko, kikosi cha uhandisi cha China cha ulinzi wa amani kilifanya usimamizi kwa nidhamu ya hali ya juu. Lakini hii ilileta matatizo kwa walinzi wa amani wa China waliokabiliwa na matatizo ya lugha, na hali ya mazingira isiyo nzuri sana.

Ili wawezesha wa amani wawe na maisha mazuri wakati wa mapumziko, kikosi cha uhandisi kilijenga maktaba ndogo yenye vitabu 6000, na VCD nyingi. Aidha, Ofisa wa utamaduni Bw. Qing Hao aliwafundisha askari wote ujuzi aliyopata katika masomo yake ya siasa katika Chuo Kikuu cha ulinzi na teknolojia. Mbali na hayo, tangu kikosi hicho kiwasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kilifanya maonesho ya michezo ya sanaa kila mwezi.

Kikosi kingine cha matibabu cha China pia kiliondoa matatizo mbalimbali yaliyokikabili na kusifiwa na wenyeji wa huko. Kikosi hicho kilijifunza kutokana na uzoefu wa vikundi viwili vilivyopita, na kuzingatia sana utunzaji kwa wagonjwa. Katika hospitali yao, kila mgonjwa ana daktari wake anayeshughulikia matibabu yake. Kazi ya daktari huyo si kama tu ni kupima ugonjwa na kutoa matibabu, bali pia wanaongea na wagonjwa na kuondoa matatizo yao wakiishi kwenye sehemu ya kigeni, hata desturi za chakula za kila mgonjwa zinaandikwa kwenye ubao wa kituo cha wauguzi, ili kukidhi mhitaji yao. Mbali na hayo, uwezo mkubwa wa madaktari na wadi safi zinaifanya hospitali ya China kama ni nyumbani kwa walinzi wa amani walioumwa. Mlinzi wa amani wa Kenya aliyepatwa na ugonjwa usioweza kutibika alitakiwa kupelekwa kwenye hospitali nyingine, lakini aliomba kubaki kwenye hospitali ya China, alisema kuwa, "Napenda hospitali ya China, na naamini hopitali ya China tu." Hayo ni maneno yake aliyowaambia madaktari wa Kikosi cha matibabu cha China kabla ya kuondoka kwake.

Hospitali ya China si kama tu inakaribishwa na walinzi wa amani walioumwa, bali pia inausaidia tume maalum ya Umoja wa Mataifa kuondoa matatizo. Siku moja, mkulima wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo alijeruhiwa mguu kutokana na ajali iliyosababisha na gari la ya Tumewa Umoja wa Mataifa. Lakini tume hiyo haiwezi kumtibu kutokana na kutothibitishwa ni upande gani utawajibika na ajali hiyo. Kwa upande mwingine, mkulima huyo hakuwa na uwezo kulipia matibabu, na hospitali ya kienyeji pia haina uwezo wa kufanya matibabu. Kutokana na hali hiyo, ofisa mwandamizi wa tiba wa Tume maalum ya Umoja wa Mataifa aliomba msaada wa hospitali ya China, na mkulima huyo alipelekwa kwenye hospitali ya China. Baada yakupimwa, waliona mfupa wake ulikuwa umevunjika, na kulikuwa na uwezekano mkubwa kuwa atakuwa mlemavu katika siku za baadaye. Aidha, mkulima huyo alikuwa na ugonjwa mwingine unaoweza kuwaambukiza watu wengine kwa kupitia damu, hivyo ni hatari sana kwa madaktari hao kumtibu.

Ili kumwokoa kwa wakati, hospitali hiyo ya China ilimfanyia upasuaji mapema baada ya kufanya maandalizi kwa makini. Baada ya kufanya upasuaji, kikundi cha matibabu cha China pia kiliajiri watu kumfanya utunzaji kwa mgonjwa huyo. Baada ya wiki mbili, mkulima huyo alipona. Wakati alipoondoka hospitali, madaktari walimsindikiza mpaka alipopanda ndege. Mkulima huyo aliwashukuru sana, hakutarajia kaam anaweza kupona baada ya kufanyiwa upasuaji. Alisifu sana uwezo mkubwa wa hospitali ya China.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-24