Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-24 18:42:40    
China kufanya kambi ya pili ya majira ya joto ya watoto yatima wa Ukimwi

cri

Idara husika ya China tarehe 24 imetoa taarifa ikisema kuwa, kambi ya pili ya majira ya joto ya watoto yatima ambao wazazi wao walikufa kutokana na ugonjwa wa Ukimwi itafanyika mjini Beijing mwezi Agosti.

Imefahamika kuwa, kauli mbiu ya kambi hiyo ni "tukue pamoja chini ya mwangaza wa jua". Watoto yatima wa Ukimwi watatembelea sehemu za kihistoria, na kujiunga na familia zenye upendo za kujitolea, kuishi pamoja na wanafamilia, ili kuhisi uelewano na upendo kutoka kwa familia kubwa ya kijamii.

Shughuli hizo ziliandaliwa na kamati ya China inayofuatilia kizazi kipya, hivi sasa inaziandikisha familia za upendo za kujitolea .