Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-24 20:20:42    
Maua yanayotengenezwa kwa samli

cri

Maua ya samli ni sanamu zinazotengenezwa kwa samli. Samli hupatikana kutokana na maziwa mabichi ya ng'ombe na ni chakula kisichokosekana katika maisha ya kila siku ya Watibet. Wasanii wa kienyeji hutia rangi mbalimbali ndani ya samli na kutengeneza sanamu mbalimbali kama vile: mabanda ya ghorofa, milima, mito, maua, ndege, wanyama wa thamani na wa ajabu na hekaya za dini ya Kibuddha. Maua ya samli yanayotengenezwa na malama wa Hekalu la Ta'er, mkoani Qinghai ni maarufu sana.

Inasemekana kwamba mnamo mwaka 641 Binti mfamle Wen Cheng wa Enzi ya Tang alichukua sanamu ya Sakyamuni na kuingia nayo Tibet kutoka mjini Chang'an na kuitukuza katika Hekalu la Dazhao, mjini Lhasa. Katika kipindi cha katikati cha Enzi ya Ming, Zonggeba, mwanzilishi wa madhehebu ya Gelu ya dini ya Kibuddha (pia inaitwa dini ya Manjano) baada ya kufanykiwa kujifunza dini ya Kibuddha huko Tibet alifinyanga shada la maua kwa samli aliyoilimikiza katika muda aliofanya kazi ya Kibuddha, na kuliweka mbele ya sanamu ya Sakyamuni ili kuonyesha moyo wake wa uaminifu. Baadaye habari hii ilienea mpaka Lushar, mkoani Qinghai?mahali alipozaliwa Zonggeba, malama wa Hekalu la Ta'er pia walianza kutengeneza maua mbalimbali ya samli na kuonyesha hekaluni katika usiku wa tarehe 15 mwezi wa kwanza (kalenda ya mwezi) kila mwaka, ambayo ni siku aliyozaliwa Zonggeba. Maudhui na aina za maua hayo ya samli hubadilikabadilika kila mwaka, na yamekuwa moja ya sanaa za kimila za dini.

Baada ya tarehe 9 Septemba (kalenda ya mwezi) kila mwaka malama wa Hekalu la Ta'er huwa wanaanza kufanya maandalizi. Kwanza hutia rangi za madini ndani ya samli nzuri nyeupe na kufunga kwa nguvu, wakati mwingine hulazimika waipigepige kwa gongo ili samli iwe sawa na laini. Kisha huchukua vijiti vyenye urefu wa mita 0.7 hivi kuwa miimo, halafu hufunga vidonge mbalimbali vya mviringo vya katani kwa mujibu wa sanamu zitakazotengenezwa. Samli kukuu hupakwa juu yake kwanza, ndipo baadaye sanamu mbalimbali hutengenezwa. Seti moja ya sanamu za samli huhitaji jitihada za watu 20 na siku 80 kukamilishwa.

Baada ya sanamu hizo kutengenezwa malama wa Hekalu la Ta'er hutengeneza mihimili ya maua yenye kimo cha mita 60 na kuziweka sanamu hizo za samli yenye rasimu nzuri juu ya mihimili hiyo. Hivyo kundi la sanamu za samli hutengenezwa. Baadaye hutumia buli la shaba nyekundu lililotengenezwa maalumu na kumwagia maji ili kuondoa vumbi juu ya maua ya samli. Kwenye mzunguko wa mihimili pia huwa kunaning'inizwa sanamu za Kibuddha za maua, ndege na binadamu zilizofumwa kwa nyuzi za rangi. Sanamu hizo zikichanganyikana na maua ya samli huunda mandhari nzuri sana.

Usiku, taa kiasi cha elfu moja za samli juu ya meza mbele ya mihimili huwaka kwa pamoja, wafukiza ubani na udi na waumini wa dini ya Kibuddha kutoka Tibet, Sichuan, Mongolia ya Ndani na Jimbo la Qinghai huwa wanatoa vitambaa vyeupe vya hariri, kunazi, peremende na keki na kuiweka mbele ya maua ya samli, na wengine hutoa sadaka zao.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-24