Baraza la mawaziri la Israel tarehe 26 lilipitisha mpango wa kuwaruhusu wayahudi watakaoondoka kutoka sehemu ya Gaza mwezi Agosti mwaka huu wahamie kwa pamoja huko Nitzanim, sehemu ya mwambao ya magharibi ya kati ya nchi hiyo. Mpango huo una umuhimu mkubwa katika kuhakikisha utekelezaji mzuri wa sera ya Israel ya kuchukua vitendo kwa upande mmoja.
Mpango huo ulitolewa miezi kadhaa iliyopita. Wakati huo, baadhi ya walowezi wa kiyahudi walifahamu kuwa, hawana budi kuondoka kutoka sehemu ya Gaza, hivyo walizungumza na serikali na kutoa matumaini yao ya wote kuhamia sehemu ya Nitzanim. Tarehe pili mwezi Juni, serikali ya Israel iliafikiana na wawakilishi wa walowezi wa kiyahudi ikikubali kujenga vitongoji vinne katika sehemu ya Nitzanim, kuwapangia wayahudi hao kutoka Gaza. Lakini kutokana na mvutano mkubwa kati ya serikali na walowezi wa kiyahudi, mwanzoni watu wachache tu walitaka kuhamia kwa hiari, hivyo mpango huo uliahirishwa. Baadaye serikali ya Israel ilitoa onyo la mwisho, kuwataka wakazi hao watoe uamuzi katika siku saba. Chini ya shinikizo za serikali, familia 1000 za wakazi kati ya 1500 zilikubali kuhamia Nitzanim. Uamuzi huo wa serikali ya Israel umetandika njia ya utekelezaji rasmi wa uhamiaji wa wayahudi wakazi kutoka Gaza.
Kutokana na uamuzi huo, serikali itaziuzuia familia hizo ardhi kwa dola za kimarekani 125 kwa mita moja ya mraba, na fedha hizo zitatolewa kutoka fidia za serikali kwa wakazi hao.
Lakini uamuzi huo ulipingwa na baadhi ya watu, wakaona kuwa, katika sehemu ya Nitzanim, kuna sehemu ya hifadhi ya viumbe ambayo ni ya kipekee ya mwambao isiyoharibika nchini Israel, kufanya ujenzi wa kiwango kikubwa kutaharibu mazingira ya viumbe ya sehemu hiyo. Watu wengine wameona kuwa, serikali inawauzia wakazi hao ardhi kwa bei rahisi kupita kiasi, wakazi hao baada ya kuhamia huko watapata faida kubwa. Lakini waziri mkuu wa Israel Bwana Ariel Sharon alisema kuwa, kesi maalum inapaswa kushughulikiwa kwa njia maalum, serikali inapenda kulipa gharama yoyote kwa ajili ya kupunguza uchungu wa wakazi kutokana na kupaswa kuhama.
Kwa mujibu wa mpango wa kuchukua hatua kwa upande mmoja uliotolewa na Bw. Sharon, kuanzia katikati ya mwezi Agosti, Israel itaanza kuondoa walowezi wa kiyahudi kutoka vituo 21 vilivyoko Gaza na vituo vinne vilivyoko ukanda wa magharibi wa Mto Jordan. Mpango huo wa kuwahamisha wakazi kwa pamoja ulioafikiwa kati ya serikali na walowezi, una umuhimu mkubwa katika utekelezaji mzuri wa mpango huo unaochukuliwa kuwa tukio la kihistoria. Kwa upande wa walowezi wa kiyahudi, uamuzi huo si kama tu umefanikiwa kulinda maslahi yao wenyewe, bali pia umehakikisha mwendelezo wa mtaa wao, kwa upande wa serikali ya Sharon, kuondoka kwa wakazi kwa pamoja kutapunguza kwa kiwango kikubwa kipingamizi kitakachotokea wakati wa kutekeleza mpango huo, aidha kutarahisisha kazi ya kuwapangia upya wakazi hao, hivyo inastahili kulipia gharama fulani.
|