Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-27 16:16:55    
"Mtaa wa chakula cha samaki" huko Zhenjiang mkoani Jiangsu

cri

"Mtaa wa chakula cha samaki" uko kwenye kando ya Mto Changjiang, mwanzoni ulikuwa kijiji kidogo cha uvuvi, ambapo wanakijiji walifanya shughuli za kuvua samaki mtoni kizazi hadi kizazi, hadi miaka zaidi ya 10 iliyopita, baadhi ya wanakijiji walipoacha shughuli za uvuvi na kuanzisha mikahawa mingi kijijini. Mikahawa hiyo inapika chakula cha samaki mbalimbali, tangu hapo watu wanakiita kijiji hicho kuwa "mtaa wa chakula cha samaki".

Eneo la "Mtaa wa chakula cha samaki" si kubwa sana, lakini kwenye mtaa huo kuna mikahawa ya chakula cha samaki zaidi ya 70, na kila mkahawa ina pilikapilika za shughuli kwa siku. Mwendesha mkahawa wa "Yulaoda" Bibi Xu Laidi alidokeza kuwa, uendeshaji mzuri wa mikahawa yote ya mtaa huo unatokana na ubichi na uzuri wa samaki wanaovuliwa kutoka mtoni, hivyo chakula cha samaki kwenye mikahawa yote kinakaribishwa na wateja. Akisema:

Mimi mwenyewe nimekua kwa kutegemea chakula cha samaki, hivyo nawajua samaki wa aina nyingi mbalimbali.

Mpishi Ni Bin aliyefanya kazi ya upishi kwenye mtaa huo kwa miaka mingi alisema kuwa, chakula cha samaki kinachopikwa kwenye mikahawa ya mtaa huo si kama tu kinatokana na samaki wabichi, bali pia samaki wote ni mazao ya Zhenjiang, ambayo yana umaalum wa sehemu hiyo. Akisema:

Mji wa Zhenjiang uko kwenye eneo la chini la Mto Changjiang, samaki wa eneo hilo ni maarufu sana nchini China. Samaki waliorudi eneo hilo kutoka bahari ya mbali wana ladha nzuri. Katika mikahawa ya mtaa wa chakula cha samaki, watu wanaweza kuonja vyakula vingi vilivyopikwa kwa upishi wa jadi, kwa mfano, watu wa huko wanapenda kutumia maji ya mto wa sehemu hiyo kupika samaki waliovuliwa kutoka mtoni, wanaona kuwa chakula kikipikwa kwa namna hii, kinakuwa kitamu zaidi na chenye ladha asilia.

 

Zaidi ya hayo, kwenye mtaa huo wa chakula cha samaki, watalii wanaweza kuona kuwa mikahawa mingi inaendeshwa na wanakijiji wenyewe, katika mikahawa mingi, mwendeshaji, mpishi na mtumishi wote wanatoka familia moja, watalii wakila chakula katika mikahawa hiyo, wanajisikia kama ni wageni wa familia za wavuvi.

Na mikahawa mikubwa kwenye mtaa huo pia ina mitindo tofauti. Kwa mfano Mkahawa wa "Jinyufang" uliojengwa kwenye meli moja ya utalii yenye ghorofa mbili unawavutia sana watalii, watalii wakila chakula kwenye mkahawa huo huku wakiangalia mandhari nzuri ya mto wanajisikia raha mustarehe. Mwendeshaji wa mkahawa huo Bwana Qian Shuangxi alisema, huu ni mkahawa pekee uliojengwa kwenye meli, ambao aliujenga kwa mwaka mmoja kutokana na misaada ya ndugu zake wanane wa nyumbani.

Bwana Douglas Pensak kutoka Marekani ambaye amefanya kazi mjini Zhenjiang kwa miaka miwili, anapenda sana chakula cha samaki kinachopikwa kwenye mtaa wa mikahawa ya chakula cha samaki, alisema:

Chakula cha samaki kinachopikwa katika mikahawa ya hapa, sijawahi kukila nyumbani Marekani, na ni tofauti na vyakula vyote nilivyowahi kuvila, ladha yake ni nzuri sana, hivyo kila mara ninakwenda kwenye mikahawa ya huko pamoja na marafiki zangu kuonja chakula kitamu cha samaki.

Idhaa ya kiswahili 2005-06-27