Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-28 16:03:59    
Bei ya mafuta ghafi yaweka rekodi mpya

cri
Kutokana na mwelekeo wa bei ya mafuta ghafi ya bidhaa za mkataba kupanda juu wiki iliyopita, tarehe 27 bei ya mafuta ghafi kwenye soko la kimataifa iliendelea kupanda juu. Kwenye soko la New York bei ya mafuta ghafi ilizidi dola za kimarekani 60 kwa pipa, na kuweka rekodi mpya katika historia. Wachambuzi wanaona kuwa, katika miaka miwili na mitatu ijayo, bei ya mafuta kwenye soko la kimataifa huenda itaendelea kuongezeka, hali hiyo bila shaka italeta athari mbaya kwa uchumi wa dunia, jumuiya ya kimataifa inapaswa kutafuta njia mwafaka ya kuzuia mwelekeo huo.

Tarehe 27, kwenye soko la New York bei ya mafuta ghafi yanayotarajiwa kukabidhiwa mwezi Agosti iliongezeka kwa senti 70 ya kimarekani kwa pipa na kufikia dola za kimarekani 60.54 kwa pipa. Siku hiyo bei ya mafuta ghafi hata iliwahi kufikia dola za kimarekani 60.95 kwa pipa, ikiweka rekodi ya juu kabisa tangu soko hilo lianze biashara ya mafuta ghafi mwaka 1983.

Kuanzia mwaka jana, bei ya mafuta ghafi kwenye soko la kimataifa ilipanda kwa mfululizo, na dola 60 kwa pipa siku zote ilikuwa bei ya kiwango cha uvumilivu la soko la biashara la New York. Sasa kinachofuatiliwa zaidi na watu ni kuwa, kiwango hicho kinaweza kudumu kwa muda gani.

Wachambuzi wa nchi za magharibi wameona kuwa, sababu kuu iliyosababisha ongezeko kubwa la bei ya mafuta ghafi la siku hiyo ni kuwa, tarehe 26, rais mpya wa Iran Mahmoud Ahmadinejad alisema kuwa, Iran itayahimiza mashirika ya nchi hiyo kushughulika na maendeleo ya viwanda vya mafuta na kuyazuia mashirika ya nchi za nje kuwekeza katika sekta hiyo. Vyombo vya habari vya nchi za magharibi vimeona kuwa, sera hiyo itapunguza kiasi cha usafirishaji wa mafuta wa Iran. Iran ni nchi kubwa ya pili yenye mafuta na gesi asilia, pia ni nchi kubwa ya pili ya kuzalisha mafuta ghafi katika kundi cha Opec. Hivyo mabadiliko ya hali ya nchini Iran na sera yake isiyo na hakika bila shaka itaathiri bei ya mafuta ghafi sokoni.

Lakini sababu muhimu zaidi inayoathiri bei ya mafuta ni uwiano kati ya uzalishaji na mahitaji. Hivi sasa soko la mafuta la kimataifa liko katika hali ya mahitaji kuzidi uzalishaji kutokana na ongezeko la kasi la uchumi wa duniani, mahitaji makubwa ya mafuta, na uwezo mdogo wa nchi zilizosafirisha mafuta ghafi. Inakadiriwa kuwa, katika robo ya nne ya mwaka huu, mahitaji ya mafuta duniani yataongezeka kufikia mapipa 8640 kwa siku. Marekani ambayo ni nchi inayotumia mafuta kwa wingi kabisa duniani mahitaji yake ya mafuta yaliongezeka kwa asilimia 7 katika wiki nne zilizopita.

Ingawa Kundi la Opec lililochukua asilimia 40 ya usafirishaji mafuta duniani liliamua kuongeza uzalishaji wa mapipa laki tano kwa siku, lakini mwenyekiti wa sasa wa kundi hilo, ambaye pia ni waziri wa mafuta wa Kuwait, Sheikh Ahmad Fahad al-Sabah, tarehe 27 alisema kuwa, Opec huenda itazingatia kuongeza uzalishaji wa mapipa laki tano kwa siku kwa mara nyingine, lakini jumuiya ya kimataifa haina imani na uwezo wa Opec, hivyo uamuzi huo wa Opec hauwezi kufanya kazi kubwa.

Vyombo vya habari vinaona kuwa, ingawa ufanisi wa matumizi ya nishati umeinuka kwa kiwango kikubwa, na uwezo wa jumuiya ya kimataifa wa kuvumilia ongezeko la bei ya mafuta umeimarika zaidi, lakini ongezeko hilo bila shaka litaleta athari mbaya kwa maendeleo ya uchumi wa duniani. Ripoti husika iliyotolewa tarehe 27 iliainisha kuwa, kama bei ya mafuta ghafi sokoni itaendelea kupanda juu, uchumi wa dunia utarudi nyuma. Kwa hivyo jinsi ya kuzuia kupanda kwa bei ya mafuta limekuwa tatizo kubwa linaloikabili jumuiya ya kimataifa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-28