Jeshi la zamani la upinzani la Cote D'ivoire, kundi la " the new forces" na jumuia ya wanamgambo ya kusini mwa Cote D'ivoire ambayo inaoungwa mkono serikali tarehe 27 hazijaanza kusalimisha silaha kutokana na mkataba uliotiwa sahihi muda mfupi uliopita, hivyo mchakato wa kusalimisha silaha kwa pande mbalimbali za Cote D'ivoire umezuiliwa kwa mara nyingine. Vyombo vya habari vinasema kuwa, uchaguzi wa rais wa Cote D'ivoire utafanyika mwezi Oktoba mwaka huu, msimamo wa pande mbalimbali za Cote D'ivoire katika suala la kusalimisha silaha umeleta athari mbaya kwa uchaguzi wa urais, ambapo utatishia moja kwa moja mchakato wa amani ya nchi hiyo.
Mwezi Septemba mwaka 2002 Cote D'ivoire kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ingawa mwaka 2003 pande mbalimbali zilizopambana zilisaini mikataba ya amani ya Marcoussis na Accra kwa nyakati tofauti, lakini katika mchakato wa utekelezaji wa makubaliano hayo, mapambano kati ya pande mbalimbali yalikuwa yanaelekea kuwa mbaya bila kusita. Chini ya usuluhishi wa Umoja wa Afrika, pande mbalimbali za kisiasa za Cote D'ivoire zilisaini makubaliano ya Pretoria mwezi Aprili mwaka huu, ziliafikiana kwa pamoja kuhusu kusimamisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka miwili, kusalimisha silaha za pande mbalimbali za kijeshi na kufanya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
Tarehe 14 mwezi Mei, wawakilishi wa jeshi la serikali ya Cote D'ivoire, kundi la " the New Forces" na tume ya kusalimisha silaha ya Cote D'ivoire waliafikiana kuhusu wakati wa kusalimisha silaha na kutawanya wanamgambo wa pande mbalimbali, makubaliano yalieleza kuwa, kazi ya kusalimisha silaha inapaswa kuanza tarehe 27 mwezi huu, na inatazamiwa kukamilishwa tarehe 10 mwezi Agosti. Lakini tarehe 13 mwezi huu, kundi la kijeshi la " the new forces" lilitangaza kutosalimisha silaha kwa wakati, na kulilaani jeshi la serikali kupanga kufanya opresheni ya kijeshi. Msemaji wa kundi la " the new forces" tarehe 27 alisema kuwa, kundi la wanamgambo wa kusini mwa Cote D'ivoire linaungwa mkono serikali ni tishio kubwa kwa mchakato wa amani, kabla ya kushughulikia suala hilo, kundi la "the new forces" halitasalimisha silaha.
Wachambuzi walisema kuwa, kutokana na vitendo vya kundi la " the new forces", kundi hilo limevunja tena ahadi yake si ajabu. Tangu Cote D'ivoire ikumbwe na vita vya wenywe kwa wenywe mwaka 2002, kundi la " the new forces" limedhibiti sehemu ya kaskazini mwa Cote D'ivoire siku hadi siku. Kama kundi hilo litashindwa katika uchaguzi mkuu, kushikilia silaha ni uhakikisho wa kupata faida kubwa ya siasa kwake.
Ili kuanzisha tena mchakato wa amani, chini ya usuluhishi wa Umoja wa Afrika, pande mbalimbali za Cote D'ivoire zitafanya mkutano nchini Afrika Kusini tarehe 28 mwezi huu. Vyombo vya habari vinasema kuwa, pande mbalimbali zinapaswa kutumia fursa hiyo, kutekeleza makubaliano ya amani kwa msingi wa maelewano, ili kusukuma mbele tena mchakato wa amani.
Idhaa ya kiswahili 2005-06-28
|