Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-29 14:55:10    
Mradi wa kimataifa wa kinu cha majaribio ya nyuklia wajengwa nchini Ufaransa

cri
    Nchi 6 zinazoshiriki kwenye mpango wa kimataifa wa kinu cha majaribio ya nyuklia jana zilifanya mkutano wa faragha huko Moscow, mji mkuu wa Russia na kuamua kuwa kinu cha kwanza cha majaribio ya nyuklia kitajengwa huko Cadarache, mji mmoja mdogo ulioko katika sehemu ya kusini mwa Ufaransa. Hadi hapo kugombea sehemu kitakapojengwa kituo hicho kumekwisha.

    Kiongozi wa idara ya nishati ya atomiki ya Russia Bw. Alexander Rumyantsev baada ya kufungwa kwa mkutano huo aliwaambia waandishi wa habari kuwa, nchi washiriki baada ya kujadiliana kwa muda mrefu zimeamua kuwa kinu hicho kijengwe katika mji wa Cadarache nchini Ufaransa. Aliongeza kuwa pande hizo zitatunga vifungu kamili vya utekelezaji kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kuhakikisha ujenzi wa kinu hicho unaanza mapema iwezekanavyo. Japan itatoa uungaji mkono mkubwa kwa kinu hicho, endapo kinu hicho kitafaulu na kuanza kufanya kazi, Japan itapata haki ya kujentga kinu cha aina ya maonesho nchini mwake.

    Habari zinasema kuwa gharama ya ujenzi wa kinu hicho itazidi Euro bilioni 4 na ujenzi wake utatumia miaka 8 hadi 10. Nchi ya kwanza inayopata nafasi ya kujenga kinu cha majaribio ya nyukilia italipa nusu ya gharama hiyo, na asilimia 50 nyingine zitalipwa na nchi nyingine 5 kwa usawa.

    Mpango huo wa kimataifa wa ushirikiano mkubwa wa sayansi na teknolojia wa kinu cha majaribio ulitolewa na kuthibitishwa na shirika la nishati ya atomiki duniani mwaka 1985. Pande zinazoshiriki mradi huo ni pamoja na Umoja wa Ulaya, Japan, Russia, Marekani, Korea ya Kusini na China. Habari zinasema kuwa mradi huo ni mmoja wa mpango mkubwa wa ushirikiano duniani kwa kufuata mpango wa kituo cha anga ya juu, lengo lake ni kupata nishati nyingi kwa kutumia hydrogen ili kutatua matatizo ya upungufu wa nishati na uchafuzi kwa mazingira katika siku za baadaye.

    Habari zinasema kuwa hivi sasa mlipuko wa mabomu ya hydrogen ni mlipuko usioweza kudhibitiwa, endapo utafiti wa mlipuko wa hydrogen utaweza kudhibitiwa na binadamu, basi binadamu wataweza kupata nishati nyingi zaidi kwa kutumia hydrogen zilizoko katika maji ya bahari.

    Hata hivyo, mpango wa kimataifa wa kinu cha majaribio ya nyukilia ulitolewa miaka 20 iliyopita, lakini ulitekelezwa taratibu sana, usanifu wa kinu na utengenezaji wa baadhi ya zana muhimu zilimaliza kujengwa mwaka 2001. Baada ya hapo pande hizo zilikuwa katika mazungumzo kwa miaka mingi. Wilaya ya Aomori, Japan na mji wa Cadarache, Ufaransa ziliingia katika uchaguzi wa mwisho, nchi tatu za Marekani, Japan na Korea ya Kusini zinaiunga mkono Japan, wakati Umoja wa Ulaya, China na Russia zinaiunga mkono Ufaransa.

    Mji wa Cadarache wa Ufaransa ulishida kupata haki ya kujenga kituo cha majaribio ya nyukilia katika mkutano wa pande 6 uliofanyika tarehe 28 mjini Moscow, na sababu zake ni kama zifuatazo:

    Kwanza, Ufaransa ni nchi ya kwanza kwa wingi wa matumizi ya nishati ya nyukilia, teknolojia yake ya kisasa kuhusu nyukilia inaweza kutoa tegemeo la uhakika kwa usalama wa kinu hicho. Pili, kuna kituo cha utafiti wa sayansi cha idara ya nishati ya nyukilia ya Ufaransa chenye wahandisi, wataalamu wa fizikia na mafundi kiasi cha 4,000 ambao wanafanya utafiti wa kuzalisha umeme kwa kutumia nyuklia pamoja na mazingira bora ya utafiti. Tatu, Umoja wa Ulaya unaiunga mkono kwa nguvu kubwa.

    Mambo mengi na mazingira mwafaka yamefanya mji wa Cadarache nchini Ufaransa kuwa mahali pa kujengwa kinu hicho cha majaribio ya nyukilia.

Idhaa ya Kiswahili