Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-29 20:36:32    
China yaandalia michezo ya Olimpiki kwa kutumia teknolojia za juu

cri

Tangu mji wa Beijing kupata nafasi ya kuandaa michezo ya 29 ya Olimpiki miaka minne iliyopita, China ilianza kazi mbalimbali za maandalizi ya michezo hiyo, sayansi na teknolojia ni sehemu moja muhimu katika kazi hizo. Katika kipindi hiki cha leo, tunawaletea maelezo kuhusu vipi sayansi na teknolojia zitahakikisha michezo hiyo inafanyika bila matatizo.

Mji wa Beijing ulipogombea nafasi ya kuandaa michezo hiyo, uliamua kauli mbiu ya "Olimpiki ya kijani, Olimpiki ya kiteknolojia na Olimpiki ya kiutamaduni", na hii ni mara ya kwanza kutoa mtizamo wa "Olimpiki ya kiteknolojia" kwenye historia ya michezo hiyo. Naibu meya wa mji wa Bi. Lin Wenyi alipofafanua mtizamo huo, alisema:

"'Olimpiki ya kiteknolojia' ni mitizamo mitatu muhimu ya michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008, pia ni msingi muhimu wa 'Olimpiki ya kijani na Olimpiki ya kiutamaduni'. Undani wake ni kufuatilia kwa karibu maendeleo mapya ya sayansi na teknolojia, kukusanya na kuingiza mafanikio ya teknolojia ya juu kote nchini China na duniani, na kuzitumia teknolojia hizo kwenye michezo hiyo."

Muda mfupi baada ya China kupata nafasi ya kuandalia michezo hiyo, wizara ya sayansi na teknolojia na kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing zimeanzisha mpango wa Olimpiki ya kiteknolojia, na kuamua kuweka mkazo katika utafiti kuhusu ujenzi wa viwanja na majumba ya michezo, kuhakikisha usalama, teknolojia ya mazingira ya hewa, vyanzo vya maji, mawasiliano na upashanaji wa habari, na teknolojia ya michezo, na kuanzisha miradi 10 mikubwa, ikiwemo "mpango wa kisasa wa usafiri wa mabasi wa Beijing", "kielelezo cha magari yanayotumia umeme" na "mfumo wa kisasa wa utoaji wa huduma za taarifa kwa lugha nyingi".

Ili kutekeleza miradi hiyo, China imetenga fedha yuan zaidi ya bilioni 3, na maelfu ya wanasayansi wanashiriki kwenye utafiti husika. Hivi sasa, maendeleo makubwa yamepatikana katika miradi kadhaa.

Bw. Liu Bin ni mtafiti wa taasisi ya mfumo wa kujiendesha katika taasisi ya sayansi ya China. Timu ya wanasayansi wanaoongozwa naye inashiriki kwenye utafiti kuhusu mfumo wa kisasa wa utoaji wa huduma za upashanaji habari kwa lugha nyingi. Alisema:

"Tunafanya utafiti kuhusu mfumo wa kisasa wa ukalimani kwa ajili marafiki wageni watakaoshiriki kwenye michezo hiyo, mfumo huo utatumika katika zana za kielektroniki za mikononi, zikiwemo kompyuta za mikononi na simu za mikononi. Kazi zake ni kutoa huduma ya ukalimani wakati wa kujiandikisha hotelini, kutafuta taarifa kuhusu mawasiliano n.k."

wakati michezo hiyo itakapofanyika mwaka 2008, wachezaji, makocha na watalii wengi kutoka nchi mbalimbali watakuja hapa Beijing. Kama wakiweka mfumo huo kwenye kompyuta au simu zao za mikononi, lugha zao zitatafsiriwa kuwa lugha ya kichina kwa haraka na urahisi. Sasa, tunajaribu mfumo huo wa ukalimani.

Kama hivyo, lugha ya kiingereza imetafsiriwa kuwa lugha ya kichina. Lakini hivi sasa, mfumo huo bado unafanya kazi polepole kidogo. Kuhusu hali hiyo, Bw. Liu Bin alisema kuwa wanafanya juhudi kurekebisha mfumo huo ili kuufanya uwe haraka zaidi.

Imefahamika kuwa, wakati michezo ya Olimpiki ya Beijing itakapofanyika, mfumo huo utaweza kutafsiri kati ya kichina kuwa lugha nyingine nyingi. Lugha tano za Kiingereza, Kifaransa, Kirusi, Kiarabu, Kihispania zinazotumika katika Umoja wa Mataifa, pia lugha za Kijapan, Kithailand na Kiujerumani zitakuwemo.

Mbali ya kutumika katika zana za mikononi, ifikapo mwaka 2008, mfumo huo utatumika katika vituo zaidi ya 3000 vya upashanaji habari mitaani, ili kuviwezesha vitoe huduma za upashanaji habari kwa lugha nyingi, zikiwemo habari kuhusu hali ya hewa, mawasiliano, utalii na ratiba ya michezo.

Wakati maendeleo makubwa yamepatikana katika utafiti wa mfumo huo, miradi mingine mikubwa inaendelea vipi? Ofisa mkuu wa wizara ya sayansi na teknolojia ya China anayeshughulikia mpango wa Olimpiki ya kiteknolojia Bw. Du Zhanyuan alieleza:

"kwa mfano, mafanikio muhimu yamepatikana katika mradi wa magari yanayotumia umeme; mradi wa majengo ya kijani na kielelezo cha matumizi umetoa kanuni za majengo ya kijani kwa majumba ya michezo na makazi ya Olimpiki, kanuni ya kutunza maji na nishati katika majengo ya Olimpiki. Kwa ujumla, hivi sasa, miradi 10 mikubwa yote inaendelea bila matatizo."

Alisema kuwa, kupitia utekelezaji wa miradi hiyo, ifikapo mwaka 2008, asilimia 80 ya taa za mitaani mwa Beijing zitatumia nishati ya jua; magari yatakayowapokea wachezaji yote yatakuwa yanatumia umeme; Kijiji cha Olimpiki kitasimamia na kudhibiti watu wanaoingia kwenye sehemu hiyo kwa kutumia teknolojia ya kutambua sura ya mtu, ili kuhakikisha usalama wa wachezaji na makocha; watu wataweza kutazama michezo kwa kutumia simu ya mikononi ya aina ya 3G. Ofisa huyo pia alisema kuwa, katika muda wa karibu miaka mitatu kabla kufanyika kwa michezo ya Olimpiki mwaka 2008, teknolojia nyingi mpya zitatokea. Idara husika za China zitachagua kwa wakati mafanikio ya kiteknolojia yanayohusu michezo hiyo na kuzitumia kwenye michezo hiyo.

Picha Husika>>


1  2  3