Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-29 21:23:16    
Mapishi ya vipande vya nyama ya nguruwe vilivyopikwa pamoja na chumvi na pilipili manga

cri

Mahitaji

Vipande vya nyama ya nguruwe gramu 300, mvinyo wa kupikia gramu 2, wanga gramu 30, sukari gramu 25, siki gramu 15, chumvi gramu 5, pilipili manga gramu 20, mafuta gramu 500, mchuzi wa soya gramu 25

Njia

1. Osha vipande vya nyama ya nguruwe, na uviweke ndani ya bakuli moja, tia mchuzi wa soya, mvinyo wa kupikia na chumvi, korogakoroga halafu tia wanga kisha koroga koroga tena.

2. Tia chumvi na pilipili manga ndani ya sufuria, pasha moto kidogo, korogakoroga kwa haraka halafu zipakue kuwa kiungo.

3. Tia mafuta ndani ya sufuria, pasha moto mpaka yawe na nyuzi joto asilimia 50, tia vipande vya nyama ya nguruwe moja kwa moja mpaka mafuta yawe na joto la asilimia 70. Pakua na uache hadi mafuta yapoe na upashe tena. Tia vipande vya nyama ya nguruwe tena vikaange mpaka viwe na rangi ya hudhurungi, vipakue. Wakati mtakapokuwa mnakula mnaweza kuchovya vipande vya nyama ya nguruwe kwenye kiungo kilichopikwa.