Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-06-29 22:10:55    
Mkutano wa mawaziri wa fedha wa Asia na Ulaya wafuatilia uchumi wa China na suala la ubadilishaji wa fedha za Renminbi

cri

Mkutano wa 6 wa mawaziri wa fedha wa Asia na Ulaya umefanyika hivi karibuni huko Tianjian, kaskazini mwa China, ambapo maofisa waandamizi wa fedha kutoka nchi wanachama 39 za Asia na Ulaya pamoja na wajumbe wa mashirika ya fedha ya kimataifa walifanya majadiliano kuhusu masuala mengi, na wamefuatilia sana masuala yanayohusiana na China.

Zaidi ya miaka 20 iliyopita, uchumi wa china siku zote umedumisha ongezeko la zaidi ya asilimia 9 kwa mwaka, China imekuwa moja kati ya nchi zenye ongezeko la kasi zaidi la uchumi duniani. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, waziri mkuu wa China Wen Jiabao alipotoa risala alisema:

China ikitekeleza sera ya kuzifungulia mlango nchi za nje na kutekeleza hatua mbalimbali za mageuzi imepata ongezeko la kasi na utulivu la uchumi kwa kutegemea juhudi zake yenyewe, maendeleo ya China yanasaidia utulivu na usitawi wa sehemu iliko China, pia yanasaidia amani na maendeleo ya dunia, na hayawezi kuwa tishio na athari dhidi ya nchi nyingine yoyote.

China inapojiendeleza, pia inafuata njia mbalimbali kwa kuchangia siku hadi siku maendeleo ya dunia. Mkurugenzi wa idara ya fedha ya kimataifa ya Korea ya kusini Bwana Tae-kyun Kwon alipohojiwa na mwandishi wa habari alisema, maendeleo ya China yana umuhimu kwa ongezeko la uchumi wa Asia na wa dunia. Alisema:

Uchumi wa China umekuwa na nguvu kubwa zaidi siku hadi siku, China imekuwa mhusika muhimu katika kuendeleza uhusiano kati ya Ulaya na Asia, na umuhimu wake pia umeonekana dhahiri katika maendeleo ya uchumi wa dunia. Korea ya kusini ikiwa nchi jirani ya China inatumai kuwa China itaonesha umuhimu mkubwa zaidi katika maendeleo ya uchumi wa dunia.

Kutokana na nguvu ya athari ya China kwa uchumi wa dunia inayoimarika siku hadi siku, hivyo kila hatua ya serikali ya China katika sekta ya uchumi imefuatiliwa sana na nchi mbalimbali duniani. Hivi karibuni jumuia ya kimataifa inafuatilia zaidi suala kuhusu mageuzi ya ubadilishaji wa fedha za Renminbi. Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, China siku zote ilitekeleza sera ya ubadilishaji wa fedha za Renminbi kutokana na dola za kimarekani, lakini kutokana na kushushwa bila kusita kwa thamani ya dola za kimarekani hivi karibuni, nchi kadha wa kadha zinaitaka China ibadilishe utaratibu wake wa hivi sasa wa kubadilisha fedha za Renminbi, na kutekeleza utaratibu wenye unyumbufu zaidi, tena zinaitaka China ikamilishe mageuzi katika muda mfupi. Kwenye mkutano huo wa mawaziri wa fedha wa Asia na Ulaya, waziri mkuu wa China Wen Jiabao amesisitiza tena msimamo wa serikali ya China kuhusu suala hilo. Alisema, China itafanya mageuzi hayo kutokana na mahitaji ya maendeleo ya uchumi wake, wakati huo huo mageuzi hayo yatazingatia ipasavyo athari yake kwa uchumi wa nchi jirani na dunia.

Waziri mkuu Wen alisema, kila nchi ina haki ya kuchagua utaratibu na sera kuhusu ubadilishaji wa fedha zinazolingana na hali halisi ya nchi hiyo. Kudumisha utulivu wa kimsingi wa ubadilishaji wa fedha za Renminbi kwenye kiwango halali na uwiano, kunasiadia maendeleo ya uchumi wa China, pia kunasaidia maendeleo ya uchumi wa nchi jirani na sehemu iliko, na kusaidia utulivu wa fedha na maendeleo ya biashara ya kimataifa.

Msimamo wa serikali ya China umekubaliwa na wajumbe wengi waliohudhuria mkutano huo. Waziri wa fedha wa Japan Sadakazu Tanigaki alisema:

Suala la mageuzi ya ubadilishaji fedha za Renminbi lingeamuliwa na serikali ya China yenyewe, idadi ya jumla ya uchumi wa China ni kubwa sana, ongezeko lake ni la kasi, sera ya uchumi inapaswa kuamuliwa na China yenyewe.

Idhaa ya Kiswahili 2005-06-28