Serikali ya Marekani tarehe 30 ilisema kuwa itashughulikia kwa makini kuhusu rais mteule wa Iran Bw. Mahmoud Ahmadinejad kuhusiwa kuwa huenda alishiriki kwenye tukio la kuukalia ubalozi wa Marekani nchini Iran na kuwateka nyara maofisa wa ubalozi huo mwaka 1979. Athari ya shutuma hizo kwenye uhusiano kati ya Marekani na Iran usio mzuri inastahili kufuatiliwa.
Habari kutoka vyombo vya habari likiwemo Gazeti la New York Times la Marekani tarehe 30 mwezi Juni vilisema kuwa, Wamarekani watano waliotekwa nyara mwaka 1979 walipoona picha ya rais mteule wa Iran Bw. Ahmadinejad walisema kuwa, aliwahi kushiriki kwenye tukio la utekaji nyara. Mwaka 1978, harakati kubwa za kuipinga ukoo wa kifalme wa Pahlavi zilitokea nchini Iran. Mwanzoni mwa mwaka 1979, Mohammed Reza Pahlavi aliondoka kutoka Iran na kukimbilia nchi za nje. Baadaye serikali ya Marekani ilimkubali Bw. Pahlavi kupata matibabu nchini Marekani bila kujali upinzani wa serikali ya Iran. Iran haikuridhika na jambo hilo. Tarehe 4 mwezi Novemba mwaka 1979, wanafunzi mia kadhaa wa Iran waliounga mkono mapinduzi ya kiislamu walikalia ubalozi wa Marekani mjini Tehran, na kuwateka nyara maofisa 52 wa ubalozi huo kwa siku 444. Baada ya tukio hilo kutokea, Iran na Marekani zilisimamisha rasmi uhusiano wa kibalozi.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bw. Scott McClellan aliviambia vyombo vya habari kuwa, Ikulu ya Marekani inashughulikia kwa makini kuhusu Wamarekani wengi kusema kuwa Bw. Mahmoud Ahmadinejad alishiriki kwenye tukio la utekaji nyara. Alisema kuwa, serikali ya Marekani inafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo, ili kugundua ukweli wa mambo.
Msaidizi wa Bw. Mahmoud Ahmadinejad mwenyewe alikanusha jambo hilo. Alisema kuwa, Bw. Ahmadinejad hakushiriki kwenye tukio hilo, na alipinga kuwateka nyara maofisa wa ubalozi wa Marekani kwani alifikiri kuwa Iran ikifanya hivyo, dunia nzima itaipinga Iran. Habari zinasema kuwa, Bw. Ahmadinejad aliwahi kuvipinga vitendo vya kuukalia ubalozi wa Marekani na kuwateka nyara maofisa wa Marekani, lakini baada ya kiongozi wa Iran Bw. Ayatollah Khomeini kusema kuwa anaunga mkono vitendo hivyo, Bw. Ahmadinejad hakupinga tena, lakini hakushiriki kwenye tukio hilo.
Wakati huo huo, baadhi ya Wamarekani waliotekwa nyara walisema kuwa hawawezi kujua kama Bw. Ahmadinejad alishiriki kwenye tukio hilo. Mmarekani mmoja aliyeteka nyara alisema kuwa, alikumbuka tu kuwekewa bunduki mgongoni, lakini hawezi kukumbuka sura ya mtu aliyemwekea bunduki hiyo. Wanasaikolojia kadhaa wa Marekani pia walishuku kuhusu Wamarekani kadhaa kumlaani rais mteule wa Iran kushiriki kwenye tukio la utekaji nyara. Walisema kuwa, miaka 25 ni muda mrefu, kumbukumbu nyingi zimepotea.
Mwaka 2002, jaji mmoja wa Marekani alipinga hukumu ya kuitaka Iran kulipa dola la kimarekani bilioni 33 kwa tukio la utekaji nyara. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia ililikataa shitaka hilo, na kuona kuwa inakwenda kinyume na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Marekani an Iran, na itaharibu heshima ya Marekani. Lakini kutokana na Wamarekani watano waliotekwa nyara kusema kuwa Bw. Ahmadinejad alishiriki kwenye tukio la utekaji nyara, baadhi ya Wamarekani wameanza kutaja jambo hilo tena, na kuona kuwa wizara ya mambo ya nje inatakiwa kutozuia shitaka la kuitaka Iran ilipe pesa kwa tukilo la utekaji nyara.
Rais George W. Bush wa Marekani alipojibu maswali ya waandishi wa habari alisema kuwa, shitaki hilo limeonesha masuala mengi. Lakini pia alisema kuwa, hatafuatilia masuala hayo kwani Bw. Ahmadinejad ameteuliwa kuwa rais wa Iran. jambo analofuatilia ni kuwa, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani lazima zihakikishe zinajulisha Bw. Ahmadinejad kuwa Iran haiwezi kuendeleza silaha za nyuklia.
Wataalamu kadhaa wamesema kuwa, wanafunzi wengi wa Iran walioshiriki kwenye tukio la utekaji nyara sasa wanashiriki kwenye mambo ya kisiasa. Baadhi yao wamekuwa maofisa wa serikali ya sasa wanaounga mkono mageuzi, na baadhi yao wamekuwa wabunge. Hivyo kama Bw. Ahmadinejad alishiriki kwenye tukio la utekaji nyara au la si jambo muhimu, mambo muhimu zaidi ni kuwa atachukua njia gani ya kidiplomasia na sera gani kuhusu Marekani.
Lakini kutokana na Ikulu ya Marekani kusema kuwa itashughulikia kwa makini shutumu husika, bado tunatakiwa kusubiri maendeleo ya jambo hilo.
Idhaa ya Kiswahili 2005-07-01
|