Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-01 18:32:21    
Ujumbe wa ukaguzi wa vyama tawala vya nchi 9 za Afrika wasifu sera ya China ya mageuzi na ufunguaji mlango

cri
    Ujumbe wa vyama tawala vya nchi 9 za Afrika wenye watu zaidi ya 20 kutoka kutoka Shelisheli, Rwanda, Cameron, Guinea Ikweta, Togo, Madagascar, Guinea, Niger na Djibouti wanafanya ukaguzi wa siku 16 hapa Beijing na kwenye mikoa ya Heilongjiang na Shandong nchini China kuanzia tarehe 21. Kwenye konglamano la vyama vya China na Afrik lililofanyika tarehe21, Juni hapa Beijing.

    Wajumbe wa ujumbe wa ukaguzi wa vyama tawala vya nchi 9 za Afrika tarehe 21 walihudhuria kongamano la vyama vya China na Afrika lililofanyika hapa Beijing, ambapo wengi wanaona kuwa, uzoefu wa mageuzi na ufunguaji mlango wa China unastahili kuigwa, uzoefu huo umekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea.

    Kwenye kongamano hilo, katibu mkuu wa ofisi ya utafiti wa sera ya Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China Bwana Ji Yushang alifahamisha vilivyo vitendo halisi na uzoefu wa China katika mageuzi na ufunguaji mlango, maelezo yake yalivutiwa sana na wageni wa Afrika, wengi wao walitoa maoni yao juu ya masuala mengi, pamoja na utaratibu wa uchumi wa soko huria wa ujamaa, uhusiano kati ya uchumi wa umilikaji wa umma na uchumi wa umilikaji usio wa umma, sera ya uzazi wa mpango, maendeleo ya kilimo, huduma za jamii za watumishi wa kampuni binafsi, uhusiano kati ya Chama cha kikomunisti cha China na vyama vinane vya kidemokrasia, na kujiendesha kwa sehemu za makabila madogo madogo.

    Kiongozi wa ujumbe huo wa ukaguzi ambaye pia ni katibu wa mambo ya nje wa Ofisi ya siasa ya taifa ya Nasara ya Chama cha maendeleo ya jamii ya taifa cha Niger Bwana Abibu alisifu kongamano hilo ambalo linahusiana na mambo mengi mbalimbali, ambayo yanalingana sana na mahitaji ya vyama vya Afrika. Alisema, baada ya kufahamishwa, wameelewa historia na hali ilivyo sasa ya mageuzi na ufunguaji mlango wa China pamoja na mwelekeo wa maendeleo yake katika siku za mbele.

    Bwana Abibu ametoa mwito kuwa Afrika na China zinapoimarisha maingiliano kati ya serikali na vyama, zinapaswa kuimarisha zaidi mawasiliano kati ya wananchi ili kuongeza maelewano kati ya wananchi wa pande hizo mbili.

    Naibu spika wa Bunge la Guinea Duaramu alisema kuwa, Guinea ni nchi inayotegemea kilimo, na zaidi ya 90 % ya idadi ya watu wa Guinea ni wakulima. Alisema, baada ya kushiriki kwenye majadiliano, amefahamu uzoefu wa China katika kuendeleza kilimo, na uzoefu huo unaweza kuisaidia sana Guinea.

    Wajumbe zaidi ya 20 kutoka Shelisheli, Rwanda, Cameron, Guinea Ikweta, Togo, Madagascar, Guinea, Niger na Djibouti wameshiriki kwenye kongamano hilo kutokana na mwaliko wa Idara ya mawasiliano na nje ya Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China, ambapo watafanya utafiti, majadiliano na ukaguzi wa siku 16 nchini China.

    Mbali na Beijing, ujumbe huo wa ukaguzi pia utakwenda kwenye mikoa ya Helongjiang na Shandong kutembelea mashirika ya kitaifa, mashirika binafsi, sehemu za uendelezaji wa uchumi na teknolojia pamoja na sehemu za mipakani zinazofanya biashara na miradi ya kilimo nchini China.

    Imefahamika kuwa, shughuli za utafiti, majadiliano na ukaguzi za pande mbalimbali za vyama vya China na Afrika zilianzishwa mwaka 1998. Katika miaka 7 iliyopita, maofisa waandamizi zaidi ya 100 kutoka nchi 24 za Afrika walibadilishana maoni na viongozi wa chama na serikali wa China kuhusu masuala mengi, na kubadilishana uzoefu wa kazi na maofisa wa ngazi mbalimbali wa chama cha kikomunisti cha China.

    Maofisa wa vyama vya utawala vya nchi za Afrika tarehe 22 waliendelea kushiriki mkutano wa utafiti na majadiliano wa maofisa wa vyama tawala vya China na Afrika uliofanyika hapa Beijing. Maofisa hao wameona kwa kauli moja kuwa, China ni mwezi wa ushirikiano wa Afrika anayeweza kuaminiwa na kutegemewa, jambo muhimu la ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika ni kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja, maofisa hao wana matumaini makubwa juu ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika ili kuleta heri na baraka kwa wananchi wa China na Afrika.

    Mjumbe wa Shelisheli alipotoa hotuba alisema kuwa, utandawazi wa uchumi duniani ni fursa pia ni changamoto kwa Afrika, Afrika inapaswa kutafuta manufaa na kukwepa madhara. Aliainisha kuwa, nchi za magharibi zinapotoa teknolojia kwa Afrika zinanyang'anya maliasili nyingi za Afrika. Hivyo nchi mbalimbali za Afrika si kama tu zinahitaji bidhaa za China zenye bei nafuu na sifa nzuri, bali pia zinahitaji zaidi kutumia teknolojia za China kwa kuendeleza maliasili zao, ili kujitoa hatua kwa hatua kutoka hali ya kuzitegemea nchi zilizoendelea za magharibi.

    Mjumbe wa Rwanda alisema kuwa, tangu kuanzishwa kwa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2000, baraza hilo limekuwa baraza linalosaidia China na Afrika kuzidisha urafiki na kupanua ushirikiano wa kunufaishana. Ili kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika, anatumai kuwa China itahamasisha mashirika ya China yaende Afrika kuwekeza vitega uchumi na kuendeleza shughuli zao, ifanye juhudi za kuongeza uagizaji bidhaa kutoka bara la Afrika; isamehe madeni ya nchi za Afrika ili kusaidia nchi za Afrika zitimize maendeleo endelevu; na isaidie Afrika kuwaandaa wataalam wa aina mbalimbali.

    Mjumbe wa Niger alisema kuwa, hivi sasa bidhaa zilizouzwa na nchi za Afrika kwa China nyingi bado ni bidhaa za hatua ya mwanzo. Anatumai wanaviwanda wa China waende Afrika kuanzisha viwanda vya ubia, kutoa teknolojia za kisasa za uzalishaji bidhaa na kutoa uzoefu wa usimamizi ili kuongeza thamani ya nyongeza nguvu za ushindani za bidhaa za Afrika zinazouzwa kwa China.

    Kutokana na takwimu zilizotolewa kwenye tovuti ya wizara ya biashara ya China, mwaka 2004 China iliongeza uagizaji bidhaa kutoka Afrika kwa asilimia 87.2 kuliko mwaka 2003; na thamani ya bidhaa za China zilizouzwa kwenye soko la Afrika iliongezeka kwa asilimia 35.7 kuliko mwaka 2003.

    Aidha, chini ya Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, serikali ya China ilianzisha "Mfuko wa uendelezaji wa maliasili za nguvu kazi za Afrika" ili kutoa nafasi za mafunzo ya aina mbalimbali kwa watu elfu 10 wa Afrika toka mwaka 2004 hadi mwaka 2006.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-01