Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-01 19:02:31    
Mafanikio dhahiri yapatikana katika juhudi za Umoja wa Afrika katika suala la amani

cri

Chini ya usuluhishi wa Umoja wa Afrika, maendeleo makubwa yamepatikana katika mazungumzo ya amani ya Cote d'ivoire tarehe 29 Juni, ambapo serikali ya nchi hiyo na jeshi la upinzani vimefikia makubaliano kuhusu kuvunja kundi linaloiunga mkono serikali na jeshi la upinzani. Hii imeonesha kuwa matokeo mazuri yamepatikana katika juhudi za Umoja wa Afrika katika suala la amani ya nchi hiyo. Bila kujali kama ahadi yao itatimizwa au la, mazungumzo ya amani ya kuvunja hali ya mvutano na hali ya Darfur inayoelekea kwa utulivu, yote hayo yametoa mchango mkubwa kwa mkutano wa wakuu wa Umoja wa Afrika utakaofanyika hivi karibuni.

Bara la Afrika limekuwa likisumbuliwa na vurugu za vita katika miaka mingi iliyopita. Kuanzia miaka ya 60 ya karne iliyopita hadi sasa, vita au migogoro 30 hivi ilitokea barani Afrika, ambapo watu milioni 7 walikufa katika vurugu za vita, na hasara za kiuchumi zilifikia dola za kimarekani bilioni 250.

Baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika badala ya Umoja wa nchi huru za kiafrika mwaka 2002, Umoja wa Afrika umeshiriki kikamilifu katika usuluhishi wa migogoro katika sehemu za Burundi, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Cote d'ivoire na Sudan. Katika mwaka mmoja uliopita, Umoja wa Afrika ulipata "mavuno" makubwa katika juhudi zake kwa ajili ya amani, na mafanikio yake ya kusuluhisha mgogoro nchini Cote d'ivoire na kutuma kikosi cha ulinzi wa amani chenye watu 2700 kukalia Darfur, yote hayo yameonesha kuwa Umoja wa Afrika umepevuka zaidi katika kushughulikia migogoro.

Mgogoro wa Cote d'ivoire na suala la Darfur ni masuala yanayofuatiliwa zaidi barani Afrika. Jaribio la mapinduzi lililotokea mwezi Septemba mwaka 2002 liliitenganisha Cote d'ivoire kuwa sehemu mbili, ambapo jeshi la serikali lilidhibiti sehemu ya kusini, na jeshi la upinzani lilidhibiti sehemu ya kaskazini. Ingawa pande mbili zilizopambana za Cote d'ivoire zilisaini makubaliano ya amani, lakini mwaka jana jeshi la serikali lilituma ndege kupiga mabomu medani ya kaskazini mara kwa mara, hivyo hali ya amani ilizidi kuwa mbaya kwa dharura.

Akiwa amekabidhiwa jukumu na Umoja wa Afrika, rais Thabo Mbeki wa Afrika ya kusini alikwenda Cote d'ivoite mara nyingi kufanya usuluhishi na kuhimiza pande mbili zilizopambana zifanye mazungumzo ya amani nchini Afrika ya kusini, na kufikia makubaliano ya amani mwezi Aprili, jeshi la upinzani lenye askari zaidi ya elfu 42 na wanamgambo elfu kadhaa wanaoiunga mkono serikali watasalimisha silaha. Lakini kuanzia mwezi Aprili, migogoro iliyotokea kwa mfululizo katika sehemu ya magharibi ya Cote d'ivoire, na mwanzoni mwa mwezi Juni jeshi la upinzani lilisema kuwa halitatekeleza ahadi yake ya kusalimisha silaha kuanzia tarehe 27 Juni. Na hali ya kufurahisha ni kuwa, pande zilizopambana za Cote d'ivoire tarehe 28 Juni zilifanya tena mazungumzo ya amani nchini Afrika ya kusini, na kufikia makubaliano kuhusu kusalimisha silaha za jeshi la kuiunga serikali kabla ya tarehe 20 Agosti ambapo jeshi la upinzani litavujwa na askari wake watarudi nyumbani hatua kwa hatua.

Mbali na mgogoro wa Cote d'ivoire, mgogoro kwenye sehemu ya Darfur, Sudan pia unapungua siku hadi siku. Msuluhishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan tarehe 29 alisema huko Khartoum kuwa, hivi sasa vifo vya raia wa sehemu ya Darfur vimekuwa chini sana ya kiwango cha hatari. Ingawa majeshi mawili ya upinzani ya sehemu hiyo hayakupata maendeleo makubwa katika mazungumzo kati yao nchini Nigeria, lakini hali ya Darfur imeelekea kuwa ya utulivu kwa udhahiri.

Umoja wa Afrika ukiwa nguvu moja kuu ya kuhimiza amani ya barani Afrika unakua siku hadi siku na kuonesha umuhimu wake wenye juhudi kwa ajili ya kutimiza amani ya Afrika.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-01