Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-01 18:41:59    
Singapore na Malaysia zasherehekea kwa shangwe miaka 600 tangu Zheng He afunge safari baharini

cri

 

Miaka 600 iliyopita, mwanabahari wa Enzi ya Ming ya China Zheng He aliongoza kikosi kikubwa kilichoundwa na merikebu zaidi ya 200 na askari na maofisa zaidi ya elfu 27 kufunga safari kutoka Taicang mkoani Jiangsu, China na kusafiri baharini mara 7. Tokea afanye safari yake ya kwanza mwaka 1405 hadi safari yake ya mwisho ya mwaka 1433 ambapo alifariki dunia akiwa njiani kurudi nyumbani, katika muda mrefu wa miaka 28, Zheng He na kikosi chake cha merikebu walipita nchi na sehemu zaidi ya 30 duniani, na kutia mizizi ya amani, ujirani mwema na urafiki. Ili kuadhimisha miaka ya 600 ya safari ya Zheng Hen na kikosi chake cha merikebu, Singapore na Malaysia ambapo Zheng He na kikosi chake waliwahi kuzipitia, hivi karibuni zimefanya shughuli mbalimbali za kuadhimisha.

Tarehe 30 juni, sherehe ya kuzinduliwa kwa "Kijiji cha utamaduni cha Zheng He" iliyoendeshwa na Idara ya utalii ya Singapore ilifanyika huko Marina Promenade nchini Singapore.

Kwenye ufunguzi wa sherehe hiyo, waziri wa mambo ya nje wa Singapore Bwana George Yeo alisema kuwa, ingawa muda mrefu wa miaka 600 umepita, lakini historia ya safari baharini ya Zheng He mpaka sasa bado inafuatiliwa sana na watu wengi duniani. Akisema:

Hivi sasa watu wana hamu kubwa na Zheng He, sababu muhimu ni kuwa watu wa dunia nzima wana kiu kubwa ya amani ya dunia nzima. Zheng He wa Enzi ya Ming ya China alifanya safari baharini ni tofauti kabisa na vitendo vya maharamia wa wakati ule wa Hispania na Ureno pamoja na mambo ya kidiplomasia ya kimizinga yaliyofanywa na Uholanzi na Uingereza, wananchi wa Asia ya kusini mashariki mpaka sasa bado wanamheshimu sana Zheng He, heshima hiyo sio kuwa ilitokana na amri yake, bali kutokana na vitendo vyake vya kishupavu na upendo na heshima ya dhati ya watu kwa Zheng He.

Bwana George Yao anaona kuwa, katika hali ya utandawazi wa uchumi duniani, nchi mbalimbali zinapaswa kuheshimiana tofauti ya kila upande, kama alivyofanya Zheng He miaka 600 iliyopita.

Mkuu wa jimbo la Java ya kati la Indonesia aliyealikwa kuhudhuria sherehe hiyo alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema kuwa, Zheng He ni mwanabaharia mwadilifu na balozi wa amani. Akisema:

Zheng He alifunga safari kutoka nchini China na alifika sehemu nyingi ikiwemo Java ya kati, hii ilikuwa safari kubwa isiyo ya kawaida. Katika safari yake aliwaletea watu wa nchi nyingine ufundi, biashara na utamaduni, pia alitia mbegu za urafiki, haya ni matokeo ya dhahiri.

Wakati huo huo, Malaysia pia imefanya shughuli mbalimbali za kuadhimisha miaka 600 ya safari baharini ya Zheng He. "Maonesho ya utamaduni wa Zheng He" yatafunguliwa tarehe 5 Julai huko Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia. Katika mji wa kale wa kihistoria Malacca, makundi ya wamalaysia wenye asili ya kichina na wataalamu wa utafiti pia walifanya maonesho ya picha na kongamano kuhusu safari baharini ya Zheng He. Naibu mwenyekiti wa Ukumbi mkuu wa mikutano wa China wa Malacca Bibi Chen Reiyan aliyefaulu kuendesha "kongamano la Zheng He" alisema kuwa, safari baharini ya Zheng He inastahili kusifiwa kuwa ni safari ya amani na urafiki. Akisema:

Mfalme wa enzi ya Ming ya China alimtuma Zheng He kwenda nchi mbalimbali, lakini hakuzitia shinikizo dhidi ya nchi nyingine, tena hakufanya unyang'anyi wa kiuchumi, safari ya Zheng He ililenga kuzitaka nchi nyingine ziiheshimu China tu. Lengo hilo ni la amani na urafiki zaidi kuliko vitendo vya wareno, waholanzi hata wakoloni wa Uingereza wa wakati huo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-01