Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-07-01 21:10:49    
Mswada wa marekebisho ya sheria ya kulinda haki na maslahi ya wanawake wapinga matumizi ya mabavu nyumbani

cri

Bi. Ding Li wa kitongoji cha Malianju cha mji wa Wuzhong mkoani Ningxia, ni mwanamke aliyekumbwa na matumizi ya mabavu nyumbani. Katika miaka minne iliyopita, Bi. Ding Li alikuwa akipigwa mara kwa mara na mume wake, na mara nyingi amewahi kuomba msaada kutoka kwa jamii, lakini alishindwa.

Hivi sasa matumizi ya mabavu kwenye familia limekuwa suala linalopaswa kutatuliwa kwa dharura. Mswada wa marekebisho ya kulinda haki na maslahi ya wanawake uliothibitishwa tarehe 26 mwezi Juni kwenye mkutano wa 16 wa halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China, unaweka utaratibu wa kupiga marufuku matumizi ya mabavu dhidi ya wanawake na unyanyasaji wa kijinsia.

Ripoti iliyotolewa na Shirikisho Kuu la Wanawake la China inaonesha kuwa, katika miaka ya karibuni, mashirika ya wanawake ya mikoa 31 nchini China kila mwaka yanapokea au kushughulikia kesi laki tatu za kiraia, kati ya hizo zaidi ya nusu ya kesi hizo zinahusiana na masuala ya ndoa na kifamilia, na matumizi ya nguvu nyumbani ni moja kati ya masuala makubwa yanayoshughulikiwa.

Imefahamika kuwa, hivi sasa tatizo kubwa linalowakabili wanawake katika ukiukaji wa haki na maslahi ya wanawake ni kukumbwa na matumizi ya nguvu nyumbani. Kesi za wanawake kukumbwa na matumizi ya nguvu nyumbani zinaongezeka kwa kasi, ambapo hali ya matumizi ya nguvu inazidi kuwa mbaya. Katika miaka ya karibuni, kesi za wanawake waliojeruhiwa, kupata ulemavu au kufa kutokana na matumizi ya nguvu nyumbani zinaongezeka, na kiwango cha ukatili wa matumizi hayo ya nguvu kimeinuka. Mwaka 2003 mashirika ya wanawake yalipokea mashitaka 263 ya vifo kutokana na matumizi ya nguvu nyumbani, yakiwa yameongezeka kwa asilimia 50.3 kuliko mwaka uliotangulia.

Aidha, mswada huo umethibitisha mashirika yanayojihusisha na kukinga na kuzuia matumizi ya nguvu nyumbani, ukiwekwa kuwa, idara za serikali za usalama wa umma, mambo ya raia, utekelezaji wa sheria, na jumuia zinazojiendesha au makundi ya kijamii katika shina mijini na vijijini zinatakiwa kuchukua wajibu wao wa kukinga na kudhibiti ipasavyo matumizi ya nguvu nyumbani, na kutoa msaada kwa wanawake waliokumbwa na mateso.

Mswada huo unaeleza kuwa, kama wanawake wakilazimishwa kufanya mapenzi au kutumia mabavu dhidi ya wanawake, wanawake wakitoa malalamiko, idara za usalama wa umma zinatakiwa kuwachukulia hatua za kisheria watuhumiwa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-07-01